Jumamosi 4 Novemba 2017, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na kuzungumza na Rais wa Jamhuri ya nchi ya Moldova Bwana Igor Dodon. Na mara baada ya mkutano huo amekutana na Katibu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin, akisindikizana na Makamu Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican Askofu Mkuu Antoine Camilleri.
Katika mazungumzo yao, wamesifu ushirikiano na mahusiano mema yaliyopo baina ya
nchi hizo mbili na mchango mkubwa wa Kanisa Katoliki utolewao katika jamii ya Moldava
hasa kwa njia ya jitihada za kiekumene na kujikita katika huduma ya elimu na upendo
kwa wahitaji.
Aidha mazungumzo yao pia yamekuwa ni kubadilisha mawazo juu ya hali halisi ya nchi
na mada mbalimbali inayohusu nchi yao ikiwa pamoja na uhamasishaji wa thamani ya familia,
amani, usalama kwa ngazi ya kikanda na Kimataifa.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |