2017-11-01 15:49:00

Papa akumbuka mashambulizi ya kigaidi huko Somalia,Afghanstan na New York!


Mara Baada ya sala ya Malaika wa Bwana Baba Mtakatifu Francisko ameonesha kwa masikitiko makubwa juu ya mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea  siku hizi katika nchi ya Somalia, Afghanstan na jana Mjini New York Marekani. Akilaani mashambulizi hayo, pia  anasali kwa ajili ya marehemu na majeruhi wote, na kuwakumbuka  familia zao. Anasema ”tuombe Bwana aweze kuongoa mioyo ya magaidi na kuokoa ulimwengu dhidi ya chuki  na uhalifu huo wa mauaji yanayotokea kwa yanatokea kwa kutaja jina la Mungu bure.

Aidha amewezasalimia mahujaji wote kutoka Italia na nchi mbalimbali. Bila kuwasahahu wajumbe wa mbio za watakatifu zilizofanyika leo hi ina kuishia katika Uwanja wa Mtaktifu Petro mjini Vatican. Tukio hilo limeandaliwa na na Chama cha Don Bosco katika Ulimwengu kwa ajili ya kuhamasishwa ukubwa wa Sikukuu ya dini kwa maana ya Sikuu ya wataktufu Wote. Amewashukuru na kuwabariki wote kuanzisha jambo hili na uwepo wao.

Halikadhalika metangaza kuwa Jumanne tarehe 2 Novemba 2017 atakwenda jioni katika makuburi ya waamerika huko Nettuno na  Fosse Ardeatine nchini Italia. Kwa njia hiyo anawaomba wamsindikize kwa sala katika ziara hizo mbili za kuwakumbuka waathirika wa vita na vugurugu. Ameongeza kusema: Vita hazai zaidi ya makaburi na vifo na ndiyo maana amependelea kufanya ishara hiyo ya kwena katika makaburi mahali ambapo anasema, inaonesha kuwa binadamu hajifunzi somo na wala kutaka kujifunza.

Kufuatia na shambulio la kigaidi huko mjini New York taarifa kutoka vyombo vya habari vinasema, mamia ya wakazi wa New York wameshiriki katika gwaride la kuadhimisha siku ya marehemu saa chache baada ya dereva wa lori dogo kuwagonga na kuwauwa watu 8 na kuwajeruhi zaidi ya 12 siku ya Jumanne tarehe 31Oktoba 2017. Meya wa jiji la New York Bill de Blasio akizungumza na waandishi habari amesema "kufutana na habari tulizonazo kwa wakati huu, hili ni tukio la kigaidi, na hasa ni kitendo cha uwoga cha kigaidi kilichowalenga raia wasio na hatia."

Gavana wa New York Andrew Cuomo ameeleza shambulio hilo limetekelezwa na mtu mpweke, akisema hakuna ushahidi unaoonesha lilikua sehemu ya mpango mkubwa zaidi. Tukio hilo lilitokea katika njia ya wapita baiskeli na watu wanaotembea kwa miguu karibu na eneo la makumbusho ya World Trade Center kusini mwa kisiwa cha Manhattan, kulikotokea mashambulio ya kigaidi ya Septemba 11, 2001.

Kamishna wa polisi wa New York James O'Neill amasema ilikua karibu saa tisa za jioni wakati dereva akiwa na lori dogo alipopita katika njia hiyo ya kupita baiskeli, akiwagonga watu wanaopita . Polisi wanamueleza dereva huyo Sayfullo Saipov ni mhamiaji mzaliwa wa Uzbekistan, mwenye umri wa miaka 29 mweney makazi yake katika jimbo la Florida. Naye Rais Donald Trump katika ujumbe kwenye ukurasa wake wa twitter ameandika, "Haijabidi kuruhusu ISIS kurudi, au kuingia nchini kwetu baada ya kuwashinda huko Mashariki ya Kati na kwengineko. Imetosha."
Hata hivyo Wizara ya Usalama wa ndani umeimarisha usalama katika jiji la New York na kuruhusu gwaride la kuadhimisha Haloween kuendelea kwa kusema Marekani haitotishwa na magaidi.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

 

 

 

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.