2017-10-31 15:21:00

31 Oktoba ni siku ya kuhitimisha maadhimisho ya miaka 500 ya mageuzi


Tarehe 31 Oktoba 2017 ni siku ya mwisho ya maadhimisho ya kumbukumbu ya pamoja ya mageuzi. Tunatoa shukrani kubwa kwa zawadi za kiroho na kitaalimungu tulizopokea kwa njia ya mageuzi. Hii ni kumbukumbu ya kushirikishana, siyo tu kati yatu bali hata kwa wenzetu wa umoja wa kiekuemeni ulimwenguni na wakati huo huo , tunaomba msamaha wa makosa yetu, kwa jinsi ambayo wakristo wamejeruhi Mwili wa Bwana, hasa kashfa za pamoja kwa miaka 500 ya tangu kuanza kwa mageuzi hayo hadi leo hii”
Huo ni ujumbe uliotolewa na Shirikisho la Kiluteri Duniani na Baraza la Kipapa kwa ajili ya Uhamasishaji wa Umoja wa Wakristo, wakati wanafunga  maadhimisho ya kukumbukumbu ya miaka 500 ya mageuzi.

Katika ujumbe huo unaendelea kwamba, Wakatoliki na Waluteri wanatambua wazi hatua za kiekumene zilizofanywa pamoja kwa miaka 50. Hija hiyo imeongozwa na sala za pamoja , maadhimisho mbalimbali matakatifu na mazungumzo ya kiekumene. Mambo hayo yameweza kutoa vizingiti vya mteto na kutokulewana na kudumisha ulewa zaidi wa pamoja ili kuweza kufikia makubaliano ya dhati ya kitaalimungu. Kwa njia ya  mwanga wa baraka hizo nyingi za  mchakato wa hatua ndefu, wanasema, hawana budi kuamsha nyoyo zao na kutoa  shukrani kwa Mungu mmoja wa Utatu kwa neema alizojalia.
Wanakumbuka matukio mengi muhimu yaliyofanyika tangu ufunguzi wa maadhimisho hayo tarehe 31 Oktoba 2016, kwa sala ya pamoja wakatoliki na waluteri  huko Lund Sweden, wakishiriki ndugu wote wa Kiekumene. 

Baba Mtakatifu Francisko na Askofu Munib A. Younan (wakati huo bado  alikuwa Mwenyekiti wa Shirikisho la Kiluteri ulimwenguni), wakati wa huduma ya kiliturujia walisaini Mkataba wa pamoja wa kujizatiti katika kuendelea pamoja na hija ya kiakumene kuelekea umoja ambao Yesu aliomba (Taz Yh 17,21). Hata hivyo siku hiyo pia ilifanya  huduma ya kukumbuka wale wenye kuhitaji msaada na mshikamano, mahali ambapo walitaka kuongeza nguvu  zaidi kwa kuandika barua yenye iliyotiwa saini na Caritas Internationalis na Shirikisho la Kiluteri dunia.

Baba Mtakatifu Francisko na Mwenyekiti Younan walitoa wito kwa pamoja wakisema: “watu wengi katika jumuiya zetu wanataka kupokea Ekaristi katika meza moja, kama kielelezo hai cha umoja wa kweli. Tufanye uzoefu wa mateso na kushirikishiana maisha yao, wale ambao hawawezi kushiriki uwepo wa ukombozi wa Mungu katika meza ya ekaristi. Tunatambua uwajibikaji wetu wa pamoja katika uchungaji kujibu kiu na njaa ya kiroho kwa watu wetu ambao ni umoja katika Kristo. Tunatamani kwa shahuku kubwa kuona majeraha  haya ya Mwili wa Kristo yanaponywa. Hilo liwe lengo na jitihada za kiekumene ambazo zinafanya maendeleo na wajibu wa mazungumzo ya kitaalimungu”.

Ujumbe unaendelea;  kati ya baraka nyingi zilizopatikana kwa kipindi  cha mwaka wa kukumbumbu ya miaka 500 ya Mageuzi, kwa mara ya kwanza Waluteri na Wakatoliki wameona Mageuzi haya kwa mtazamo wa kiekumene. Kumbukumbu hii imeweza kuleta uelewa mpya juu ya  matukio ya karne ya XVI yaliyosababisha  mgawanyiko huo. Kwa njia hiyo upo utambuzi hawali ya yote ya kwamba wakati uliopita hauwezi kubadilika tena walakini,  matokeo yake juu yetu yanaweza kubadilisha namna  ya kukua kwa umoja na ishara ya matumaini katika ulimwengu huu. Ni matumaini ya kushinda mgawanyiko na utofauti wa vikundi vikundi. Kwa maana  hiyo ni kutafuta zaidi ya kile kinachotuuunganisha kuliko kile kinachotenganisha. Upo utambuzi wa Mkataba wa pamoja wa mafundisho ya haki uliotiwa saini na Shirikisho la Kiluteri duniani na Kanisa Katoliki mwaka 1999, ambao pia ulisainiwa hata na Baraza la Kanisa la Wametodisti Duniani mwaka 2006, na kwa mwaka huu wa kukumbukumbu ya Mageuzi kusainiwa na Muungano wa Mageuzi ya Makanisa Ulimwenguni.


Leo hii Mkataba huo unapokelewa na kutambuliwa rasmi  na Umoja wa Waanglikana katika Sikukuu ya Hitimisho ya Miaka 500 ya Mageuzi inayofanyika katika  Monasteri ya Westminster Uingereza. Kwa msingi huo Jumuiya za kikristo zinaweza kujenga daima uhusiano mkubwa kwa maana ya kiroho na ushuhuda wa pamoja katika huduma ya Injili.  Kwa upeo wa maisha ya baadaye,ni kujikita zaidi kuendelea na hija hiyo ya pamoja inayoongozwa na Roho wa Mungu kuelekea katika kukua kwa umoja uliopendwa na Bwana wetu Yesu Kristo. Na kwa Mungu Mmoja katika nafsi tatu  kuwa na roho ya sala , katika lengo zaidi  la kung’amua tafsiri ya Kanisa, Ekaristi, na huduma yake, aidha kujikita zaidi ili kufikia malengo ya umoja kamili. Yeye aliye anzisha kazi hii ataipeleka hadi siku ya Bwana Yesu Kristo. (Fil 1,6).

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.