2017-10-30 09:14:00

Vatican:Kalenda ya Maadhimisho ya Baba Mtakatifu kwa miezi ijayo


Ziara ya Kitume nchini Cile na Peru kuanzia tarehe 15 -22 Januari 2018, Misa ya tarehe 2 Novemba katika Makaburi ya waamerika Nettuno na Siku ya Masikini  Duniani  tarehe 19 Novemba katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.
Ni baadhi ya matukio katika ratiba ya Baba Mtakatifu Francisko iliyotolewa mapema karibuni kwa miezi kuanzia Novemba, Decemba 2017 na Januari 2018 iliyothibitisha katika Kalenda ya maadhimisho ya Baba Mtakatifu ktuoka katika Ofisi ya Maadhimisho ya Liturujia Vatican.
 
Baba Mtakatifu ataadhimisha misa ya kumbukumbu ya waamini marehemu huko Nettuno Italia tarehe 2 Novemba 2017, baadaye, tarehe 3 Novemba ataadhimisha misa nyingine katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwa ajili ya kukumbuka makardinali na maaskofu marehemu waliofariki kwa kipindi cha mwaka huu.
 
Tarehe 19 Novemba anatarajiwa kuadhimisha misa Takatifu kwa ajili ya Siku ya Maskini Duniani, aliyoitangaza mwishoni wa mwaka wa Jubilei ya huruma, na wiki itakayofuata kuanzia tarehe 26 Novemba hadi 2 Desemba, ataanza ziara yake ya kitume nchini Myanmar na Bangladesh.
 
Tarehe 8 Desemba 2017 ni sSkukuu ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya asili Baba Mtakatifu kama utamaduni, antarajiwa kwenda kuweka shahada la maua katika sanamu ya Mama Maria kwenye uwanja wa Hispania Roma, na tarehe 12 Desemba ataadhimisha Misa Takatifu ya Bikira Maria wa Guadalupe, msimamizi wa Bara la Marekani. Misa zote kipindi cha Krismasi kama utamaduni zitafanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Misa ya mkesha wa Krismasi tarehe 24 Desemba itaanza saa tatu na nusu za usiku masaa ya Ulaya, na sikukuu ya Epifania itafanyika tarehe 6 Januari 2018.
 
Jumapili tarehe 7 Januari, Baba Mtakatifu ataadhimisha Misa Takatifu ya sikukuu ya Ubatizo wa Bwana katika Kanisa la Sistina, mahali ambapo atawapa sakramenti ya ubatizo baadhi ya watoto. Na maadhimisho ya mwezi Januari yatafungwa huko Cile na Peru mahali ambapo anatarajia kuanza ziara ya kitume kuanzia tarehe 15 hadi 22 Januari 2018.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
 
 








All the contents on this site are copyrighted ©.