2017-10-30 08:58:00

Papa Francisko anasema Wakristo waipe roho mpya bara la Ulaya !


Kumbuka Ulaya ambayo haijatengenezwa na namba bali na watu. Wakristo wote wa  Ulaya wajenge jamii inayosimama juu ya binadamu na jumuiya. Ni msisitizo wa Baba Mtakatifu katika hotuba yake aliyotoa jioni ya tarehe 28 Oktoba kwenye Mkutano wa Kamati ya Baraza la Maaskofu Ulaya katika mada ya kuifikiria Ulaya. Mkutano umefanyika kwa lengo la maadhimisho ya miaka 60 ya mkataba wa Roma kwa ajili ya Ulaya.

Mchango Mkubwa ambao unaweza kutolewa na wakristo wa Ulaya leo hii ni ule wa utambuzi ya kwamba siyo tu idadi za katiba bali Ulaya imetengenezwa na watu. Ametoa hotuba hiyo kwa washiriki wa Mkutano 350 katika Ukumbi Mpya wa Sinodi wenye kauli mbiu  juu ya kufikiria Ulaya. Mchango wa Kikristo katika nyati zijazo za mipango ya Ulaya.

Mkutano huo umeudhuliwa na makardinali, maaskofu, mabalozi na wawakilishi kutoka katika mashirika ya kikristo, ili kujadili kwa pamoja Mkutano ulioandaliwa na Baraza la Maaskofu wa Ulaya na Tume ya Kamati ya Jumuiya ya Ulaya. Baba Mtakatifu amewaonesha njia, kwamba msingi wa Ulya ni watu na jumuiya kama wakristo wanaotaka na ambao wanaweza kutoa mchango mkubwa na kuijenga Ulaya.
 Matofari ni mazungumzo, ushirkishwaji, mshikamano maendeleo na amani. Aidha amekumbusha kuwa thamani msingi ambayo wakristo wameichukua hadi sasa ni maana ya utu ambao ni mfano wa Mungu.
 
 Akichambua zaidi, ametoa mfano wa Mtakatifu Benedikto, Baba Mtakatifu anasema, binadamu siyo tena kuwa ni rahisi kuwa  mzalendo au mtumishi wa utawala wa usiku, wala kuwa bidhaa ya kubadilisha na kuwa kazi. Kwa mtazamo wa Benedikto anasema hakuna kutoa nafasi hiyi, bali yupo binadamu, lakini kwa bahati mbaya Baba Mtakatifu anaendelea kusema, leo hii hakuna wafanyakazi wapo wale wanaonesha uchumi, hakuna wahamiaji, wapo wanaodai fedha, kwa maana wanataka  namba tu.
 
Kuwa na sura inakulazimisha kuwajibika, kwa njia hiyo wakristo wanapaswa kukumbuka kuwa zaidi ya yote Ulaya ni imetengenezwa na watu ili waweze kugundua maana ya ushiriki wa jumuiya, na kupinga tabia za kuishi kiupweke, kwa kufikiria kuwa ni mantiki ya uhuru ambao ni kufanya uishi kipekee. Kwa mujibu  wa Baba Mtakatifu anasema, hili ni jambo la hatari. Wakristo wanatambua  utambulisho wao zaidi ni ule wa kujenga familia ambayo ni msingi na ndiyo sehemu ya kugundua utambulisho huo. Muungano utofauti kati ya mke na mme ambao kama ni wa kweli, unatoa matunda, na uwezo wa kujifungua maisha na kwa wengine. Jumuiya hai inatambua kwa dhati kupokea kila aina ya tofauti bila ubaguzi na kutoa matunda  mpya katika, kazi, ubunifu na utamaduni
 
Kutoka Kaskazini, kusini, mashariki na Magharibi, Ulaya ni lazima iwe sehemu ya mazungumzo anasema Baba Mtakatifu kama ilivyokuwa zamani, na siyo tu nafasi ya kuichumi bali moyo wa kisiasa.kwa maana hiyo Baba Mtakatifu anawaalika kufikiria nafasi chanya iliyo nayo dini katika jamii na kwamba inawezekana mazungumzo ya kidini kati ya wakristo, waislam Ulaya. Aidha anabainisha hatari zaidi ya mawazo potofu yanayojitokeza juu ya thamani ya dini katika maisha ya umma. Mara nyingi sauti ya mazungumzo mema ugeuka kuwa kelele za kulipiza visasi. Na hiyo imejitokeza katika baadhi ya nchi, kwa maana hiyo wakristo wanaalikwa kukuza mazungumzo ya kisiasa yaliyo mema kwa kutoa hadhi kisiasa ili iweze kuwa huduma kwa ajili ya mema ya wote.
Akielezea maana ya uongozi pia Baba Mtakatifu anasema, kuwa kiongozi leo hii inahitaji mafunzo, kujiandaa vema na uzoefu, kwa maana hiyo, Ulaya inapaswa iwenafasi muhimu ya kutoa thamani ya utofauti, kwa mtazamo wa wahamiaji kwamba ni rasilimali badala ya kuonekana kuwa ni mzigo wa kutupilia mbali. Kwa upande mwingine anasema viongozi wanapaswa kuwa makini katika suala linalohusu uhamiaji, kwa maana hiyo, wasijenge kamwe kuta bali mchakato ambao pia unatoa sheria. Na kwa upande wa wahamiaji lazima wafuate na kuheshimu sheria na kukubali utamaduni wa nchi inayowapokea. Kujikita kwa ajili ya jumuiya inayoshirikiana maana yake ni ujenzi wa nafasi ya mshikamano na siyo tu upamoja wa vikundi vidogo vya kujinufaisha. 

Ni lazima kuwa na ukarimu kwa wadhaifu na kuwasaidia kizazi kijacho. Tangu miaka ya 60 migogoro ya kizazi inaendelea bila kukosa, anabainisha na kueleza, siyo tu kwa upande wa Ulaya kukosa watoto bali wengi wa watoto wamenyimwa haki ya kuzaliwa kwasababu pia kugundua uweze wa kukabidhi vijana nyenzo na utamaduni wa kukkìabiliana na wakati endelevu. Ulaya inaishi kwa namna nyingine kwa ukosefu wa kumbukumbu, kwa njia hiyo inapaswa kugunda thamnai ya wakati uliopita, ili kutajilisha wakati uliopo na kuwakabidhi kizazi kijacho matumaini. Vijana wengi wanajikuta wamepotea njia mbele ya ukosefu mizizi na upeo, wakati huo huo elimu inapaswa kujikita katika jumuiya nzima
 
Ulaya inaitwa kuwa chemi chemi ya maendeleo kamili kama vile alivyokuwa anafikiria Mwenye heri Papa Paulo VI: Inahitajikita kazi na hali inayostahili katika kazi. Mfano unaweza kuwa kwa wakristo waajili ambao kwa karne iliyopita walianzisha makampuni ili kuweza kutoa ajira yenye hadhi kazini; kuanzisha kwake hata leo hii inahitajika katika ulimwengu wa utandawazi usiokuwa na roho, ambao umeunda magunia mengi ya unyonyaji na umasikini. Hii inahitaji watawala wa nchi wa kuweza kuanzisha mzunguko wa fadhila hii, anaongeza Baba Mtakatifu, na hiyo ianzie katika uwekezaji wakitazama familia, elimu na kuwawezesha maendeleo na amani ya jumuiya nzima ya raia.
 
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
 








All the contents on this site are copyrighted ©.