2017-10-27 09:44:00

Papa amezungumza na wana anga moja kwa moja wakiwa juu angani!


Ni nafasi ipi aliyo nayo mwanadamu katika ulimwengu? Je kuna maana gani ya kuita nguvu ya upendo unaotoa msukumo? Ni kitu gani kinasukuwa kuwa mwana anga? Je mnaishije katika nyumba iliyozungukwa na vioo wakati huo huo inazunguka yenyewe ? Je ni muhimu gani wa kushirikiana katika misioni hiyo?  Hata hivyo nyinyi ni nyumba ndogo ya vioo ambayo ukamilifu wake ni mkubwa katika ukubwa wa sehemu.
 Hayo ndiyo maswali na maelezo ambayo Baba Mtakatifu Francisko  ametoa wakati wa mahojiano, kwa muda wa dakika 25, pamoja na wafanyakazi wa Kituo cha Kimataifa cha Anga, waliko sasa katika obiti. Baba Mtakatifu ameuliza maswali kwa wanasayansi hao sita katika katika kazi hiyo tarehe 26 Oktoba 2017.

Baada ya maswali hayo , jibu lakwanza limetolea ma mwana anga Paulo Nespoli wa Italia na kwamba majadali huo ni nyeti sana kwani  utafiti huo  unawafanya kutafakari kwa kina juu ya upeo na mipaka ya ulimwengu. Lakini pamoja na hayo unatoa maswalimengi ya kujiuliza , je tunatoka wapi na  tunakwenda wapi? . Lengo letu ni kujua utu wetu na kujaza maarifa yetu. Ningependelea ameongeza, watu kama yeye na siyo wahandisi na fizikia tu bali hata wanataalimungu, wanafalsafa, waandishi wa mashairi wangeweza kufika huko kwenye Obiti. Katika kuongelea juu ya upendo na ulimwengu, Baba Mtakatifu amekumbuka mstari maarufu wa mtunzi kwa vitabu wa kizamani nchini Italia Dante, ambaye anahitimisha katika kitabu chake mstari usemao, "upendo unaotingisha jua na nyota"; hivyo amewauliza wanasayansi hao nini maana ya kuita upendo  nguvu inayohamisha ulimwengu.

Katika swali hili, amejibu mwana anga kutoka Urusi Alexander Misurkin ambaye ametumia kitabu kingine kiitwacho “Mfalme mdogo” kilichoandikwa na Antoine de Saint Exupery. Ni historia ya kijana mdogo ambaye yuko radhi kutoa maisha yake kwaajili ya kuokoa mimea ya ardhi. Kwa maana nyingine amejibu upendo ni ile nguvu yenye  uwezo wa kutoa  maisha kwa ajili ya mwingine.
Swali la tatu Baba Mtakatifu ametaka kujua zaidi, kwa maana ameuliza sababu za kuwafanya wawe wana anga. Ni Mwana anga mwingine kutoka Urusi Segey Ryazanskiy, amesema tendo la kuwa mwana anga, limetokana na  kuiga  babu yake, aliyekuwa ni mhandisi katika misioni ya Sputnik 1, wakati huo mwana anga kutoka Marekani, Randy Bresnik, yeye amesisitiza juu ya uwezekano wa kuona ardhi kidogo kwa macho ya Mungu, kuona uzuri wa sayari hii.

Kubadilisha mtazamo: Swali la nne lilikuwa linahusu juu ya safari angani, na kwamba kusafiri angani, mara nying unabadilisha mambo  mengi anasema Baba Mtakatifu, ambayo kwa maisha ya kawaida huyapatii uzito wake, kwa mfano juu ya wazo kusema au kutazama “juu” na “chini”. Kuna jambo Baba Mtakatifu anasema, kuishi katika Kituo cha kazi katika anga mnapata  mshangao? Anaongeza, hiyo ni kutokana na kushangazwa na  ni jibu la Marko T. kwa maana alivyokabiliana na jambo la mtazamo tofauti ambao yeye binafsi anafikiri kwamba ni wa kifamilia. Ili kujua mahali ulipo baba Mtakatifu anaongeza, ni lazima kuamua binafsi  ni wapi juu na chini ili kuweza kukaa katika ulimwengu huo mdogo.

Umuhimu wa ushirikiano ilikuwa pia suala msingi kwa wanaanga hao, ambapo Baba Mtakatifu amesema, jamii yetu ni yenye ubinafsi, badala yake, anasema, katika maisha jambo muhimu ni ushirikiano.  Je mnaweza kutoa mifano nyeti ya ushirikiano kati yenu mnayojikita  katika kazi angani?.
Mwana anga Joseph Acab amesema, kituo hicho cha tatifi angani ni mfano mkubwa wa ushirikiano Kimataifa, hivyo kwa pamoja anasema, tunaweza kufanya mambo mengi na bora ambayo ni vigumu kufanya peke yako.

Mwisho Baba Mtakatifu Francisko , amewashukuru wana anga hao, na kwamba anahisi kuwa ni wawakilishi wa familia ya binadamu katika mpango wa tafiti kwenye  nafasi ya anga. Mwanaanga Nespoli amemshukuru kwa niaba ya wenzake watano ya kwamba, ameweza kuwainua tena juu na kuwatoa katika shughuli zao za kila siku za kiteknolojia na kuwafanya wafikirie mambo makubwa zaidi kwa ajili ya maisha yao.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.