2017-10-24 17:00:00

Papa:Tambua vema kiini cha Fumbo la Yesu Kristo Msulibiwa kwa ajili yako


Kiini cha fumbo la Yesu Kristo ni kwamba alinipenda na kujitoa yeye mwenyewe afe kwa ajili yangu. Ni manano ya Baba Mtakatifu Francisko aliyo yatoa wakati wa mahubiri ya Siku ya Jumanne 24 Oktoba 2017 katika kikanisa la Mtakatifu Marta Mjini Vatican ambapo anatafakari Mateso ya Bwana na njia ya msalaba ili kuweza kuingia katika fumbo hilo. Baba Matakatifu anasema, ndiyo unakwenda katika  misa, unasali , na unakuwa  mkristo mwema lakini kiini cha swali la kujiuliza je kweli umeingia katika fumbo la Yesu Kristo.

Akitazama  kutoka Somo la Kwanza la Mtakatifu Paulo kwa Waroma , Baba Mtakatifu anabainisha kuwa Paulo anatumia maneno ya dhambi, kutotii, neema na msamaha  akitaka tutumbue jambo lolote. Kwani anajisikia kuwa ni muhimu kueleza kila ambacho anataka kusema. Lakini nyuma ya hayo yote lina historia ya wokovu. Kutokana na ukosefu wa maneno ya kutosha kuelezea  Kristo, Paulo anatusukuma kwa nguvu zaidi ili tuweze kutumbukia katika fumbo la Kristo.

Maneno hayo , Baba Mtaktifu anasema ni katika hatua ya safari ya kuingia kwa kina katika fumbo lake Kristo , ambalo siyo rahisi kulitambua,  kwa maana  uzito huo ni mkarimu na mabao siyo rahisi kutambua kwa majadiliani ya kijujuu tu  hadi kufikia  mwisho wake. Bali ili kutambua Yesu ni nani kwa ajili yako au kwa ajili yetu, Baba Mtakatifu anaongeza inahitaji kujita kwa kina zaidi  kutambua fambo lake.

Katika somo jingine la Mtakatifu Paulo anasema ,”yeye alinipenda na kujitoa yeye mwenyewe kwa ajili yangu”.Baba Mtakatifu anabainisha kuwa, inatambulika wazi hata kama yupo ambaye ni tayari kufa kwa ajili ya mwenye haki , lakini ni Yesu peke yake anayetoa maisha kwa ajili mwenye dhambi kama mimi. Na katika maneno hayo Mtakatifu Paulo anatafuta njia ya kuweze kuingia katika fumbo lake Kristo, kwa maana siyo rahisi inahitaji neema, anaongeza Baba Mtakatifu.

Baba Mtakatifu anasema, waliotambua hilo siyo tu watakatifu waliotangazwa , bali hata wakatakatifu wengi wanaojificha katika maisha yao ya kila siku, watu wanyenyekevu, wenye kuwa na matumaini kwa Bwana.Hawa wamejikita kwa kina katika fumbo la Yesu Kristo msulibiwa, ambapo Mtakatifu Paulo kitendo hicho anakiita cha wehu, lakini anasema, iwapo anataka kujisifu  kwa jambo lolote, yeye anajivunia dhambi zake na Yesu Msulibiwa , Baba Mtakatifu anaongeza, anajifuvunia dhambi zake na siyo kisomo chake na Galamaliele katika Hekalu au jambo jingine.

Akifafanua juu ya  jambo jingine la kufanya utambua fumbo la msalaba anasema ni kutazama kwa undani zaidi dhambi binafsi. Iwapo unaingia kanisani ndiyo unatambua kuwa Yesu yupo katika Neno, Yeye anakuja lakini hiyo tu haitoshi kuweza kuingia katika fumbo anasama Baba Mtakatifu ni kujitafakari nafsi ya dhambi zako na kutazama Yeye tu.

Aidha anasema, ili kuingia katika fumbo la Yesu Kristo, lazima kujiachia kabisa katika huruma, mahali ambapo hakuna maneno, kuna mkumbatio wa upendo. Upendo uliompleke hadi mauti kwa ajili yangu na  yetu. Baba Mtakatifu ametoa mfano mmoja kuhusu   kuungama dhambi ya kwamba, unapoungama dhambi na Mungu anakuhurumia, lakini  bado haijatosha kuingia kabisa ndani ya fumbo la Yesu. Ni lazima kutambua kwamba ninakwenda kukutana na Yesu na kuingia kabisa katika fumbo lake,katika mikono yake na msamaha wake anao sema Mtakatifu Paulo kuwa ni zawadi ya msamaha wa bure.

Ni vema kufanya njia ya msalaba, ni kufanya njia ya msalaba nyumbani ukifikiria mateso Bwana. Hata  mababa wakubwa wa kiroro walikuwa wakishauri daima kuanza maisha ya kiroho kwa makutano ya fumbo la Yesu Msulibiwa. Mtakatifu Teresa aliwambia watawa wenzake kuwa, yeye kabla ya kufika katika sala ya pamoja , alikuwa tayari amesha fanya tafakari ya Mateso ya Bwana. Msalaba wa Yesu Kristo ndiyo unapaswa kufikiriwa na kutafuta njia moyoni mwako na   kuwa  na uhakika  kuwa Yeye mwenye alinipenda na akatoa maisha yake kwa ajili yangu.

 Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya kiswahili ya radio Vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.