2017-10-23 15:00:00

Papa:Sisi sote tu mfano wa Mungu hivyo tumpe yaliyo yake Mungu


Baba Mtakatifu akitafakari Injili ya Jumapili ya 29 ya Mwaka kutoka Mt 22,15-21 amekazia juu ya uhusiano wa Mungu na wanadamu na hasa pale Yesu anapoulizwa juu ya kulipa ushuru kwa mfalme wa Roma Kaisari, nia yao ilikuwa ya kutaka kumweka kwenye mtego, lakini yeye anawajibu kwa utulivu juu ya swali hilo kwamba wampe Kaisari yaliyo ya Kaisari na Mungu yaliyo ya Mungu.
Baba Mtakatifu anasema kwa upande mwingine Bwana anataka watu warudishe kile ambacho ni chake, kwa maana kulipa ushuru siyo tendo la kuasi, huo ni wajibu wa madaraka ya nchi. Na kwa upande mwingine Yesu anaonesha ukuu  wa Mungu ya kwamba, wampe kile kilicho chake kama Bwana wa maisha ya binadamu na katika historia.

Kilelezo cha sura ya Kaisari iliyowekwa kwenye sarafu ni kuonesha kuwa naye anayo haki na wajibu na kama mzalendo wa selikali, lakini kwa upande mwingine inaonesha sura nyingine ambayo hata binadamu anayo yaani wake wa Mungu. Yeye ni Bwana wa kila kitu na sisi tumeumbwa kwa mfano wa sura yake. Yesu aliweza kuwa na swali kutokana na lile aliloulizwa na wafalisayo ambalo  ni zaidi ya mzizi  wa maswali tunayojiuliza kila mmoja, yaani mimi niko upande gani. Je mimi niko katika upande wa familia, wa mji , wa marafiki, shule , kazi , siasa au serikali? Hakika ndiyo. Lakini zaidi ya hayo Yesu anafundisha kuwa sisi ni watu wa Mungu, kwa sababu tupo kwa neema yake na kile tulicho nacho kinategemea yeye tu. Kwa maana hiyo  katika maisha yetu ya  kila siku hatuna budi kumshukuru Mungu, na kutambua sehemu msingi tunayopaswa kuwapo utambuzi wa roho kulekea kwa Baba anaye muumba kila mmoja kadri ya mfano wake, Baba Mtakatifu anaongeza hilo ni fumbo la kupendeza!

Mkristo amaalikwa kujikita kwa dhati katika hali halisi ya kibinadamu na kijamii bila kupinga Mungu na Kaisari, kwasababu Baba Mtakatifu anaonya kuwa inawezakana  tabia ya msimamo mkali. Kwa namna hiyo mkristo anaalikwa kuwa na juhudi za dhati, lakini akiongozwa na hali halisi kwa  Mwanga utokanao na Mungu. Jambo muhimu  la kukazania ni Mungu na matumaini, kwa maana kwa njia yake, hakuna kukwepa hali halisi, bali huo ni mwaliko wa kujibidisha kwa Mungu ambaye sisi tunatoka kwake ili kuishi maisha ya hapa duniani kwa ukamilifu na kujibu kwa ujasiri changamoto zake.
Baada ya sala ya Malaika wa Bwana, Baba amekumbusha kuwa Jumamosi, huko Barcellona wanametangazwa wenye heri Matteo Casals, Teofilo Casaius, Fernando Saperas na wenzo 106 wafiadini, wa Shirika la Watawa wa Mtakatifu Antoni Claretian walio uwawa kwa ajili ya kutetea imani yao wakati wa vita vya wenyewe wa wenyere huko Huispania.Ushujaa wao na kwa maombezi , uweze kuimarisha ukistro hata kwa nyati zetu, sehemu mbalimbali za dunia wanaoteswa na kubaguliwa.

Aidha katika fursa hiyo ameyatoa hata wito wa amani dunia, hasa akitaja nchi ya Kenya mahali ambapo kuna migogoro na mahali amabapo Baba Mtakatifu anasema alitembelea huko mwaka 2015, kwa njia hiyo  anasali ili taifa liweze kukubiliana na matatizo ya sasa katika hali ya mazungumzo yenye ujenzi, kuwa na moyo wa kutafuta mema kwa ajili ya wote katika kipindi hiki wanapojiandaa kurudia uchaguzi wa rais wa nchi tarehe 26 Oktoba 2017.

Na mwisho amewasalima mahujaji wote waliofika viwanja Mtakatifu Petro kutoka pande zote za dunia, kwa namna ya pekee mawazo yamewaendea wanajumuiya kutoka  Peru wanaoishi Roma ambao wameungana pamoja katika viwanja vya Mtakatifu Petro na Picha Takatifu ya Mama yetu wa miujiza (Señor de los Milagros”)

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.