2017-10-23 17:30:00

Papa:Mabadiliko ya hali ya hewa yanahitaji kuitikia na kutoa jibu haraka


Katika ufunguzi wa Mkutano  wa Kimataifa tarehe 23 Oktoba 2017 kuhusu Maji na Mazingira: maziwa makubwa ya ulimwengu kukabiliwa, Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican, amesoma ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko kwa wajumbe wote kutoka mataifa mbalimbali  ambapo ujumbe wa Baba Mtakatifu  unasema, mabadiliko ya hali hewa yanahitaji kuitikia kwa haraka na kutoa majibu ya haraka na yenye ufanisi.

Kwa wajumbe wote wa mkutano huo wanawaalikwa wagundue wazi juu ya zawadi yenye thamani ambayo ni maji iliyotolewa kwa maisha ya sasa na endelevu ya binadamu. Baba Mtakatifu anawataka wawe na jitihada za kuhamasisha dhamiri ya jumuiya ya kimataifa kuhusiana na matatizo ya dharura. Na sio tu kutafuta ufumbuzi wa vitendo, bali hata anasema umuhimu wa njia inayoweza kuunganishwa ili kukuza maendeleo na uelimishwaji wa utamaduni wa huduma hiyo.(Laudato si, n.231).Amemamlizia akiwatakia baraka, kwamba waongozwe na hekima ya Mungu kwa wote wanaojikita katika shughuli hizo.
Mkutano huo umeandaliwa na Wizara ya Mazingira na Ulinzi wa maeneo, kwa kushirikiana na Tume ya Uchumi ya Ulaya na Umoja wa Mataifa (Unce), Shirika la Kimataifa la Bonde la Maji (Riob), Mshikamano wa Mataifa kwa ajili ya maji na Hali ya Hewa (GAWaC), ambayo huunganisha Ushirikiano wa Biashara na Ushirikiano wa Megacity, uliyoanzishwa  UNESCO, na AquaMadre. Hii ni kwa mara ya kwanza, wahusika wengi wa bonde la mito katoka mabara yote  kukutana nchini Italia ili kujenga mjadala wenye kujenga lengo la kukabiliana na hali halisi  ya baadaye ya maji,inayotishiwa na  mabadiliko ya hali ya hewa ya mara kwa mara na ya vurugu, na mara nyingi mabadiliko makubwa kama vile mafuriko, ukame na uharibifu wa mazingira.

Majadiliano kati ya mito mikubwa duniani ndiyo itakuwa lengo kati katika mkutano huo ili apate kuwa na mtazamo mmoja wa maandalizi ya Mkutano wa Cop 23, utakaofanyika Bonn mwezi Novemba, pia Jukwaa la Maji  Duniani la  Brasilia linalotarajiwa kufanyika  mwezi wa tatu 2018. Hii ni mikutano miwili muhimu ambapo ni mategemeo kwamba maji, kwa hakika yana haki ya kutambuliwa, kama jukumu kuu katika mjadala wa hali ya hewa na  uchaguzi ambao serikali zitachukua kwa siku zijazo kwenye sayari hii.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.