2017-10-23 16:00:00

Papa: Fedha ni miungu pia ni ubatili kutegemea mali za ulimwengu huu


Katika nyakati hizi ambapo vyombo vya habari vinatoa habari nyingi za majanga na  ukosefu wa haki hasa zinatozo watazama kwa namna ya pekee watoto wadogo, tuombe Mungu kwa nguvu ili aweze kuongoa mioyo ya watu na kumjua Bwana badala ya  kuabudu miungu ya fedha . Ni maombi ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa mahubiri yake asubuhi ya Jumatatu 23 Oktoba 2017 katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta Mjini Vatican. Akitafakri Injili ya Mtakatifu Luka kuhusu mtu tajiri na mwenye fedha nyingi kutokana na kuwa na mazao mengi, Baba Mtakatifu anaweka bayana kuwa hiyo fedha ndiyo mungu wake, ndiyo  maana inatufanya kutafakri jinsi gani ilivyo ubatili mtupu kwa yule anayetegemea mali za ulimwengu huu, badala ya kutegemea tunu msingi na uhusiano na Bwana.

Mbele ya mavuno mengi aliyopata huyo mtu huyo, anafikira kujenga magala mengine, kwa maana ndiyo mawazo yake  ya kwamba yatamwongeze miaka mingi  ya kuiishi,yeye anafikiria kupata utajiri tu  hadi puani,  maana ni kutaka kushiba tu, Baba Mtakatifu anakuongeza, huo ndiyo mtindo wa ufujaji wa kutisha. Laki ni Bwana peke yake  anayeweka kikomo juu wale wanaoshikilia sana fedha, hasa binadamu anapokuwa mtumwa wa fedha. Hiyo siyo methali ambayo Yesu anatunga bali ni ukweli, ni hali halisi ya sasa anasisitiza Baba Mtakatifu. Wapo watu wengi wanaoishi kwa kuabudu fedha na kufanya fedha kuwa ndiyo Mungu wao. Watu wa namna hiyo maisha yao hayana maana. Ni kama wa mfano wa yule anayemtaja Yesu kujilimbikizia tunu binafsi bila kujitajilisha kwa Mungu kwa maana hatambui ni utajiri upi ulioko kwa Mungu.

Akindelea na mahubir hayo ametoa mfano mwinine wa matukio mbali mbali  wakati bado yuko Argentina na kuelezea juu ya  tajiri mmoja ambaye pamoja na utambuzi wa kuwa anaumwa sana , aliamua kununua nyumba nzuri sana akifikiria atajikabidhsi nayo mbele ya Bwana. Hata leo hii wapo watu wengi wenye njaa ya fedha na utajiri wa dunia hii  anasema baba Mtaktifu, watu wenye mengi lakini wanaona watoto wengi wanakufa njaa na hawana hata dawa ya kuwatibu, hawana elimu na wamebaguliwa, hiyo ndiyo kuonesha wazi juu ya kuabudu fedha maana yake ni kuua  pia kutoa kafala za kibinadamu.

Kuabudu miungu hii ni kufanya watu wengi wafe na njaa. Fikirieni kisa kimoja tu cha watoto 200,000 wa Rohingya ambao wanaishi katika makambi ya wakimbizi. Katika kambi kuna watu 800,000  na kati yao ni watoto 200,000, hawa  hawana chakula na wala madawa nathibitisha Baba Mtakatifu. Kwa njia hiyo maneno ya Bwana hayakusema tu kwa enzi zile lakini hata leo hii yanejileza katika hali halisi. Ni kusali leo na kuomba sala ya nguvu hasa iweze kugusa mioyo ya watu wanao abudu miungu fedha, lakini pia iguse hata mioyo ya kila mmoja asiweze kutumbukia katika hali hiyo bali tkutazama  na kuwajibika

Hata hivyo Baba mtakatifu pia amegusia jambo la vita hata ndani ya familia kuhusiana na fedha akitoa mfano kwamba wengi wanatambua nini kinatokea  hasa katika masuala yanayohusu urithi, familia nyingi zinagawanyika na kuishia katika chuki. Kwa namna hiyo Baba Mtakatifu anatoa ushauri kukumbuka wito wa Bwana, anayetaka tujitajilish kwake maana ndiyo njia pekee. Siyo kwamba Bwana anadharau fedha, bali anaonya yale matendo ya kushikilia fedha na kujisahau.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican 








All the contents on this site are copyrighted ©.