2017-10-20 15:12:00

Papa ameonya kuacha unafiki wa maisha! ni kuishi ukweli wa ndani


Bwana atupatie neema ya kutambua ukweli ndani, kwa maana msamaha wa kweli wa Mungu ni wa bure unaotokana na neema na utashi wake, hautokani na na nguvu zetu binafsi na kazi ya kibinadamu. Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko akifafanua Liturujia ya Neno la Mungu kutoka katika Barua ya Mtume Paulo Kwa Waroma, asubuhi ya tarehe 20 Oktoba 2017 katika Kikanisa cha Mtakatifu Martha mjini Vatican. 

Matendo yetu mema  ni jibu la upendo wa bure wa Mungu ambaye anasamehe daima na kufanya tuwe na haki. Utakatifu wetu ni ule wa kupokea daima msamaha na ndiyo maana zaburi ya siku inasema , heri aliyesamehewa dhambi, na kusitiriwa makosa yake. Heri Bwana asiyemhesabia upotovu, ambaye rohoni mwake hamna hila. Baba Mtakatifu anasema ni Bwana anayesemehe dhambi ya asili na ambaye anasemehe mara tu tunapomgeukia na kutubu kwakwe. Hatuwezi kusamehewa dhambi kwa nuzvu zetu wenyewe, bali ni yeye anasemehe,sisi tunaweza kujibu msamaha huo kwa ajili ya matendo yetu mema.

Jilindeni na chachu ya Mfarisayo, ambayo ni unafiki. Lakini hakuna neno lililositirika ambalo halitafunuliwa,wala lililofichwa ambalo halitajulikana. Basi,yoyote mliyosema gizani yatasikiwa mwangani; na mliyonena sikioni mwa mtu katika vyumba vya ndani, yatahubiriwa juu ya dari.
Katika Injili ya siku kutoka  Luka, Baba Mtakatifu anafafanua,aksema Yesu anatuelekeza kutambua njia nyingine ya kutafuta haki, akitumia picha ya wale wanaojidai kuwa watakatifu na kumbe ni wanafiki, ndani ya mioyo yao, papa nasema, ni wachafu ndani ya mioyo yao, lakini kijujuu wanataka wanaonekane wenye haki na  wema, wanafunga, wanasali au kutoa sadaka. Lakini ndani ya mioyo yao hakuna kitu, wanaishi maisha ya kinafiki, hakuna ukweli wowote ndani ya mioyo yao.

Baba Mtakatifu anabainisha kuwa watu hawa wanaishi roho ya kinafiki na kutafuta utakatifu wa kinafiki : Yesu anawaalikwa watu waishi maisha ya kweli yaani ukweli ukweli wa ndani. Kujihesbu mwenye haki ya kijujuu ni sawa na mapovu ya sabuni ambayo leo hii yapo na kesho hayapo tena.
Yesu anataka tuwe na uwiano sawa kwa maana ya  maisha ya kile tunacho fanya na kile tunachoishi ndani ya roho zetu. Uongo na unafiki uharibu mtu vibaya sana, kwa njia hiyo ni vema kujiuliza na kutubu maovu mbele ya Mungu wako. Hiyo ni tabia mbaya ambayo taratibu inajengeka na kufikia hatua za  kuwadhuru wengine. Kutubu binafsi kwa Mungu wako ndiyo njia  nzuri ya kuhepukana na unafiki na  kujifunza hekima ya kujihukumu binafsi bila kuficha dhambi zako mbele ya Mungu.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 
All the contents on this site are copyrighted ©.