2017-10-19 16:41:00

Balozi Dejan Sahovic wa Serbia awasilisha hati za utambulisho Vatican


Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi, tarehe 19 Oktoba 2017 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mheshimiwa Dejan ŠAHOVIĆ Balozi wa Serbia mjini Vatican ambaye ameoa na amebahatika kupata watoto wawili. Balozi Dejan ŠAHOVIĆ alizaliwa kunako mwaka 1955 na katika maisha na utume wake kama mfanyakazi wa Serikali amejikita zaidi katika masuala ya kidiplomasia huko Yugoslavia ya zamani, Umoja wa Mataifa. Kama mfanyakazi katika mambo ya kisiasa amewahi pia kuiwakilisha nchi yake kwa niaba ya Umoja wa Matifa huko Cambodia, Afrika ya Kusini na Tagikistan kati ya mwaka 1992 hadi mwaka 1996. Amewahi kuwa wakili kati ya mwaka 1996 hadi mwaka 2000.

Balozi Dejan ŠAHOVIĆ amewahi pia kuwa ni mshauri kwenye Wizara ya Mambo ya nchi za nje  nchini Serbia katika kipindi cha mwaka 2000. Baadaye akahamishiwa Geneva kama mwakilishi wa Serikali ya muungano kati ya Serbia na Montenegro, kwenye Makao makuu ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyoko mjini Geneva, Uswiss, kati ya mwaka 2004 hadi mwaka 2006. Baadaye akateuliwa kuwa Naibu Waziri; Mratibu wa Ofisi ya Rais wa Serbia na Kamati ya Mawaziri wa Baraza la Ulaya, nafasi aliyoitumikia hadi kufikia mwaka 2007. Baadaye, aliteuliwa kuwa Balozi wa Serbia nchini Hungaria kati ya mwaka 2008 hadi mwaka 2012; Mkuu wa Kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kati ya mwaka 2012- 2013. Kati ya Mwaka 2013 hadi mwaka 2015 alikuwa ni mwakilishi wa Serbia kwenye mkutano wa OSCE. Kuanzia mwaka 2016 amekuwa ni Balozi na Waziri wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.