2017-10-16 14:57:00

Mchango endelevu wa Wakristo Barani Ulaya


COMECE: Kufikiria tena Ulaya : Mchango wa Wakristo  kwa wakati endelevu wa Umoja wa nchi za Ulaya. Ndiyo Kauli mbiu ya Mkutano Mjini Vatican kuanzia tarehe 27-29 Oktoba  2017 wa Tume ya Maaskofu wa Jumuiya za Umoja wa  Ulaya (Comece) kwa ushirikiano na Vatican kutokana na tukio la Umoja wa Ulaya kuadhimisha kumbu kumbu ya miaka 60 tangu ulipoanzishwa kwa wakuu wa nchi mkataba wa Roma  wa tarehe 25 Machi 1957. Habari zilitolewa  na Baraza la Maaskofu wa Umoja wa wa Ulaya, zinaelezea lengo la mkutano huo kuwa ni kutaka kutafakari juu ya ujenzi na kufanya majadiliano ya kweli na wazi kati ya wadahu kutoka sehemu mbalimbali kijiografia utamaduni, dini, na  lugha katika lengo la kuhamasisha zaidi umoja katika utofauti na kiini cha mada ya hadhi ya binadamu.

Kwa lengo la mkutano unaojikita  kwa ajili ya wema wa wote ili kuweka  hadhi ya binadamu kama kiini cha maisha ya umma, washiriki wanaitwa kutazama njia mpya zinazoweza kuunganisha wadau wote  wa jamii, hasa wahusika wa dini na kisiasa. Washiriki wa mkutano huo mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea  Bunge la Umoja wa Ulaya, kuzingatia tuzo ya Charles Mkuu  na mkutano na wakuu wa nchi na wakuu wa serikali za nchi za EU, hatmaye, Baba Mtakatifu Francisko  atahutubia  washiriki Jumamosi tarehe 28 Oktoba ili naye apate  kushiriki  kweli kwa kutafakari  juu ya  maisha endelevu ya Umoja wa nchi za Ulaya  na kukumbusha  ahadi ya Kanisa katika harakati za mpango huo wa amani. Taarifa inasema, baada ya migogoro miwili ya mauti duniani, Ulaya ina wajibu wa kuelewa jukumu lake kuelekea ulimwengu na wananchi wake, kutafuta njia ya kuhusisha kikamilifu wanaume na wanawake wa nyakati zetu. Kwa njia hiyo madhumuni ya kufikiri Ulaya ni kusaidia mchakato huu wa dhamiri binafsi.

 Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.