2017-10-14 16:23:00

Ushauri wa Papa kwa wanafamilia wa Mt. Vincent wa Paulo;kuabudu ukarimu,kwenda!


Umekuwa mkutano wa furaha kubwa wa Baba Mtakatifu Francisko katika Uwanja wa Mtakatifu Petro Mjini Vatican, tarehe 14 Oktaba 2017 wakiwa waunganika familia nzima  kutoka pande zote za dunia la Shirika la Mtakatifu Vincent wa Paulo katika maadhimisho ya miaka 400 tangu kuanzishwa kwa Shirika hilo. Kauli mbiu ya Mkutano wao  "Nilikuwa mgeni mkanikaribisha".

Baba Mtakatifu katika hotuba anasema  ambukizeni upendo,matapano na uwajibikaji katika dunia. Amehutubia hayo katika umati wa wanachama karibia 2,000 kutoka pande za dunia, ambao wameungana kwa pamoja kusikiliza neno kutoka kwa papa wakiwa pia mbele ya  Masalia ya moyo wa Mtakatifu Vincenzo wa  Pauli ulio kuwa umewekwa juu ya Altare. Baba Mtakatifu anasema ni moyo ambao umeanzisha matendo ya upendo  na ambayo yatadumu milele. Kwa Matashi hayo anawatia moyo katika safari yao kama familia kutembea kwenye barabara duniani kote  kwa kutumia maneno matatu rahisi lakini muhimu: 

Kwanza anawashauri Kuabudu:  ni neno la kwanza lenye  wito na kukumbusha tabia ya Mtakatifu Vincenzo  kwa maana alikuwa anajitoa sadaka ya kila siku na  maisha ambayo ni chemichemi ya upendo unaotolewa katika dunia. Baba Mtakatifu anasema, kwa upande wa Mtakatifu Vicent wa Paulo , sala ulikuwa siyo jambo la mazoea  tu  sala ili kuwa ni kukaa mbele ya Mungu,kujiwakilisha kwake kwa urahisi na kujabidhi. Hiyo ndiyo sala ya wazi na nzuri  hasa ile ya kumpa Bwana nafasi yako  kwa kumsifu, kuabudu na hakuna cha zaidi. Baada ya kugundua nini  maana ya kuabudu,Baba Mtakatifu anasema  siyo rahisi  kuacha kwa sababu ni sala ya usafi na upendo wa kina wa Bwana ambaye anatoa  amani, furaha na kuyeyusha mahangaiko ya maisha.

Kwa njia hiyo,  kwa mujibu wa Baba Mtakatifu anathibitisha,  kuabudu ni kujiweka mbele ya Bwana kwa heshima, utulivu na kimya, kumpa nafasi ya kwanza  ukijikabidhi kwa imani, hayo ni mazoezi yanayo ambukiza. Anaye abudu kweli, anayefuata  chemichemi hai ya upendo haiwezekani asiambukizwe na upendo mkuu na kuanza kuwa na mwenendo mzuri na wengine kama afanyavyo Bwana . Yeye anageuka kuwa  mwenye huruma zaidi na utambuzi ,  wa kuwajibika na kushinda ugumu wake juu ya wengine.

Akielezea juu ya  neno la pili kwa wanafamilia wa Mtakatifu Vincent wa Pauli  anasema ni kukaribisha kwa maana ya ukarimu:  hii haina maana ya kuweka nafasi kwa ajili ya mtu,  badala yake ni ile tabia ya kuwa tayari na kujikana kwa kina anasema Baba Mtakatifu. Kukaribisha maana yake  ni hali ya kupunguza ukubwa wa nafsi yako na kuilekeza katika namna ya kufikiria, kuchukulia maisha ambayo kwanza siyo jambo binafsi pia  kutambua kuwa hakuna muda wangu.Lakini anasisitiza, hiyo ni tendo la hatua ya kwenda polepole, katika kuondoa umimi , muda wangu, kupumzika kwangu, haki zangu, mipango yangu, ratiba yangu. Anayekaribisha anajikana umimi na  kuingia katika maisha ya “wewe na “sisi”

Mkristo aliye mkarimu Baba Mtakatifu anasema, anafanya makutano bila kulalamika, anapanda amani hata kama hajulikani, huyo ni mwana kweli na mwamininfu wa Kanisa , ambaye ni Mama aliyepokea  maisha na kusindikiza. Baba Mtakatifu anatoa maombi kwa Mtakatifu Vincent wa Pauli ili saidie kuthamanisha hali hii ya kanisa  na  maisha yetu yetu yaweze kuondokana uhasama , chuki, hasira , kelele na ubaya wa kila aina (Ef 4,31).

Neno la mwisho ambalo Baba Mtakatifu anaweza kushuri wanafamilia ya Mtakatifu Vincent ni kwenda / kuondoka, neno hilo kwa maana nyingine  Baba Mtakatifu anarudia akitazama maisha ya  mwanzilishi wa Shirika hilo. Upendo hausimami  kwa maana  ni mzunguko. Baba Mtakatifu anasema , anayependa hakai katika sofa nzuri na kutazama matukio ya ulimwengu yatakayokuja na bora , bali yeye kwa shahuku  rahisi anamkwa na kuanza mwendo kuanza safari . Mtakatifu Vincent wa Pauli alisema maneno mazuri : “Wito wetu ni ule wa kwenda , siyo tu katika parokia na majimbo bali katika dunia nzima. Je kufanya nini? Ni  kwenda kuwasha moyo  wa waamini katika kutumiza kile alichofanya mtoto wa Mungu. Yeye alijuka kuleta moto katika dunia na kuuwasha kwa upendo wake.(Rej: Mkutano 30 Mei 1659)”.

Kwa njia hiyo ,mMwisho Baba Mtakatifu anatoa wito wa kutosimama katika safari yao katika barabara za dunia na kuchota upendo wa Mungu katika kuabudi na kuwasambazia wote kwa njia ya kuambukiza upendo  uwajibikaji na mapatano.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.