2017-10-14 15:22:00

Misa Vatican ya hitimisho la Jubilei ya miaka 100 ya kutokea Maria wa Fatima


Tarehe 13 Oktoba 2017 katika Kanisa la Kuu la Mtakatifu Petro wameadhimisha ya Misa ya Ekaristi Takatifu, katika hitimisha rasmi Maadhimisho ya  Jubileo ya Miaka 100 tangu Bikira Maria alipowatokea watoto wa Fatima, Francis, Yacinta na Lucia misa hiyo imeongozwa na Kardinali Angelo Comastri Msaidizi wa Papa katika Mji wa Vatican.

Kabla ya Misa Takatifu ,wameanza na maandamano ya msafara mrefu kutoka njia ya Conciliazione wakiwa wamebeba sanamu ya mama Maria wa Fatima aliyewatokea watoto  wachungaji watatu. Ni sanamu aliyoibariki Baba Mtakatifu Francisko wakati wa kuanza utume pia mwaka jana tarehe 12 Oktoba walizundua maadhimisho ya Jubilei miaka 100 ya kutokea mama Maria.

Katika maandamano hayo yaliyotayarishwa na Kanda ya Mko wa Lazio na Chama cha kuwahudumia wagonjwa nchini Italia Unitalsi wameshiriki watu wa kujitolea na wagonjwa kutoka kila kona ya mkoa wa Lazio nchini Italia,wahudumu wa Kaburi Takatifu Vatican na kuongozwa na  Bendi ya Kikosi cha Walinzi wa Vatican, kwa wimbo wa Mama Maria.

Aidha kabla ya misa Takatifu Kardinali Comastri pia ameongoza sala ya Rosari  Takatifu , akiwaalika watu wote walioshiriki kuitikia mwaliko wa Bikira Maria alioufanya kwa Mtakatifu Lucia kusali kwa ajili ya amani na uongofu wa wadhambi. Chini ya mwaliko huo huo wa kardinali pia katika mahubiri yake amepitia hatua zote za kutokea kwa mama Maria wa Fatima, hivyo  kwa njia ya maombezi ya Mtakatifu Lucia, Mama Maria atujaze utulivu kama alio uonesha katika tukio la kuwatokea watoto hao akiwa na moyo wa  umama.

Mahubiri yake  amemalizia akiwatia  moyo wote walioshiriki maadhimisho hayo na  kwamba wachukue  uamuzi wa kutembea kwenye maisha ya Injili kupitia nyayo za Yesu  kwa ajili ya kushirikiana na kuwa wema kwenye ulimwengu na ili Injili itoe msukumo wa kuelekea mbingu mpya ambayo Yesu mwenyewe amekwisha tangulia na kuandaa.

 Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.