2017-10-14 14:59:00

Baba Mtakatifu yuko karibu kiroho kwa waathirika wa moto mkali Califonia


Baba Mtakatifu Francisko anaonesha mshikamano wake kwa watu waliopatwa na janga la moto huko  Califonia nchini Marekani .Katika ujumbe wake ulio tiwa saini na Kardinali Pietro Parolin,  Katibu wa Vatican barua ikelekezwa kwa Askofu Mkuu wa Los Angeles, José Horacio Gómez na Askofu Salvatore Joseph Cordileone wa San Francisko. Baba Mtakatifu anaonesha ukaribu wake kiroho kwa sala hasa kwa wale wote waliopoteza wapendwa  wao na bado wana hofu kubwa ya maisha ya wale ambao bado hawajapatikana. Katika barua hiyo anawatia moyo hata viongozi wa raia, vikozi vya uokoaji wa waathirika katika janga hili la kutisha, wote anawatumia baraka zake za kitume.  

Watu zaidi ya 31 wameripotiwa kufariki katika moto  ulotekekeza na msitu  na nyumba  katika jimbo la Califonia nchini Marekani tangu Jumapili iliyopita. Na wengi  watu bado hawajulikani mahali walipo, wakati huo huo vikosi vya kuzima moto vinaendelea . Watu zaidi ya 5 000 wameondolewa katika mji wa Calistoga na kupelekwa mahali salama, wakati hekta za mraba 76,000 wa misitu zimekwisha teketea. Aidha taarifa inaeleza kuwa wanao husika na shughuli hii ya kuzima moto na kuokoa ni watu 8.000  hata hivyo upepo na ukame vinapelekea zoezi la kuzima moto huo kuwa gumu.

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.