2017-10-13 16:59:00

Papa amekutana na wajumbe ya Kamati ya maandalizi ya ziara ya 2015 Sri Lanka


“Ninawakaribishe kwa furaha kubwa wajumbe wa Kamati ya kichungaji kutika Sri Lanka”. Ni maneno aliyoanza nayo Baba Mtakatifu Francisko katika  Ukumbi wa Mkutano mjini Vatican,  kwa waamini 50 hivi kutoka nchini Srilanka mi Wajumbe wa Kamati ya Kichungaji ambao wako katika  ziara yao, ambao Baba Mtakatifu Francisko alikutana nao wakati wa Ziara yake ya Kitume Barani Asia Januari 2015. Baba Mtakatifu anasema, ilikuwa ni sikukuu kubwa na fursa iliyoandaliwa kwa uanglifu na mshikamano wa Baraza la Maaskofu Katoliki wa Sri Lanka.

Baba Mtakatifu amewakumbusha juu ya safari yake ,na  jinsi ya mshangao wa tembo 40 waliotoa salam kwake katika barabara ya kutoka uwanja wa ndege kuelekea mji wa Colombo. Na kwamba ilikuwa ni ziara ya saba ya kitume , kwa maana ya pili katika Bara la Asia baada ya kutembelea Jamhuri ya nchi ya Corea. Anakumbusha hata kipindi muhimu cha kihistora katika nchi hiyo. Fursa ya kutembelea nchi hiyo anasema, ilikuwa ni neema na hasa baada ya miaka mingi  ya mateso na migogoro na pia juhudi zao za kutafuta mapatano na kuponywa kwa majareha .  Anasimulia jinsi alivyofurahishwa na wazalendo wa nchi hiyo wenye utajiri wa dini, tamaduni tofauti ambao walikwenda kumpokea kiwanja cha ndege na hata barabara ya kuelekea Colombo.

Ka njia hiyo Baba Mtakatifu amegusia hatua zote za ziara yake katika siku hizo na jinsi gani alijawa nafuraha kubwa ya kumtangaza Mtakatifu Joseph Vaz , mmisionari  maalumu katika Bahari ya Hindi , aidha umati mkubwa sana walio ungana pamoja katika sala kwenye madhabahu ya mama Yetu wa Madhu  ambayo ni ishara ya ulinzi na mapatano ya Sri Lanka. Pamoja na hayo Baba Mtakatifu anawashukuru kwa namna ya pekee kwa kila mjumbe wa Kamati ya maandalizi ya ziara ya Baba Mtakatifu Francisko kwa juhudi kubwa ,na nguvu nyingi ambazo pia ziliwezesha kuonesha matunda.

Anawashukuru pia familia zao ambao walijitoa sadaka na kuwatia moyo katika kazi yao, hivyo uwepo wao leo hii mjini Vatican Papa anasema, umemfanya ajisikie nyumbani kwao na kukumbuka mambo mengi matakatifu waliyofanya kwa pamoja wakati wa ziara yake nchini mwao.
Mwisho kabla ya baraka zake, amemkabidhi wazalendo wote wa Srilanka na Serikali kwa maombezi ya Mama Yetu Maria wa Madhu. 

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.