Mahubiri ya Monsinyo Dario Vigano' Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Mawasiliano Vaitican kwa washiriki wa Kozi ya Mafunzo ya Mawasiliano huko Orvieto Italia yenye kauli mbiu "utawalwa: huduma kwa ajili ya wote" , tarehe 10 Oktoba 2017. Akitafakari somo la siku anasema, wameunganika kwa pamoja na furaha ili kustaajabia upendo wa Mungu alionao na kuendelea kutimiza ile historia ya binadamu katika maisha ya kila mmoja. Somo la siku linahusu historia ya Yona. Monsinyo anasema, Nabii Yona ni historia ya uinjilishaji. Ni Nabii mtiifu aliyetumwa kwenda kuwatangazia watu habari mjema ya kuongoka kabla ya hasira ya Mungu haijangukia kwa watu wa Ninawi kutokana na dhambi nyingi zilizotendeka, japokuwa Mungu anawavumilia kwa unyeyekevu na pia kuwatumia mtu wa kuweza kuwapa tahadhali.
Monsinyo Vigano anasema, kama asemavyo Baba Mtakatifu Francisko kuwa, Mungu hakuweza kuwatupa watu wake, hawaachi washindwe na dhambi kwa maana yeye ni mwaminifu na neema zake ni kubwa zaidi ya dhambi. Hilo ni fundisho la kujifunza kwa sababu tunavyo vichwa vigumu na hatutaki kujifunza. Lakini Mungu ni mkubwa zaidi ya dhambi, ana uwezo wa kushinda dhambi hata kubwa, za aibu, hata zile ambazo ni vigumu kuelezeka . Mungu anashinda dhambi hizo kwa njia ya upendo.
Hiyo ina maana ya kwamba Mungu anatawala na ndiyo maneno ya imani kwa Bwana ambaye
katika uwezo wake, anajinyenyekeza na kuinamia binadamu Mungu anainama kutoa huruma
na uhuru wa binadamu ambaye ameumbwa kwa mfano wake. Hiyo ni kwasababu tunapoondolewa
dhambi, tunakuwa wazuri na kuwa mfano wa Mungu hakika (Rej. Hotuba Baba Mt. 14 Desemba
2016).
Upendo wa Mungu unasamehe yote hasa anakutana na moyo wa binadamu ulio tayari funguka
kwa ajili ya kupokea neema na kutubu dhambi alizotenda. Na ndiyo historia ya mji wa
Ninawi, na ndiyo historia ya kila mmoja ambaye yuko tayari kujiachia ili akumbatiwe
na ukarimu, huruma ya Baba mwema na mwenye upendo mkubwa.
Hiyo ndiyo shule ya maisha ili upendo ulitolewa na Baba kwa njia ya mwanae, uweze
kuwa na maana katika kuishi kila siku, hasa kwa mantiki ya msamaha wa kweli na siyo
kilipiza visazi, kukaribisha na siyo kukatalia , kuwa na huruma na siyo kuwa na ugumu
wa mioyo.
Monsinyo vigano aidha anasema, neno ambalo limesikika liweze kuwa mwanga na ulazimwa
wa kutambua mabaya , kukataa ubaya huo na kutazama yaliyo mema na kukaribisha. Kwa
kufanya hivyo siku moja wote wanaweza kuimba kila siku zaburi “Sikiliza kwa makini
sauti ya kilio changu (Zab129,1-2)
Aktafakari juu ya Injili ya siku kutoka kwa Mt Luka, inaelezea juu ya Yesu na dada
wawili Marta na Maria. Monsinyo Vigano’ amesisitiza juu ya kutambua uwajibikaji katika
shughuli za kawaida na maisha ya kiroho.
Katika shughuli za kila siku, ni muhimu kukumbuka neno la Mungu kwa maana pamoja
na shughuli hizo, Yesu hajakataa , bali mi muhimu kuzingatia jambo lenye kuleta maana
hasa katika usikivu wa neno la Mungu. Kwa njia hiyo katika maisha yetu ya kila siku
yawe ni kukaa na familia, kazini au marafiki ni muhimu kukumbuka kusikiliza Neno.
Bila kufanya hivyo Monsinyo Vigano’ anasema, ipo hatari ya kuangukia kufanya kazi
na kusahau roho ikakauka, mwisho wake ni kusahau yale mambo muhimu ya maisha ambayo
yanakufanya uweze kuishi na kukabiliana na chamoto za kila siku.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |