2017-10-06 09:22:00

Miaka 25 ya amani nchini Msumbiji kwa njia ya Jumuiya ya Mt.Egidio


Ilifahamika  kuwa ni amani ya Italia  kwa kile cha kuadhimisha miaka 25 tangu kumalizika kwa vurugu nchini Msubiji. Mwaka 1992 Jumuiya ya Mtakatifu Egidio ilianza kujihusisha na nchi hiyo ili kuweza kuondokana na vuruguvu, kwanza  wapate uhuru wake kutoka kwa Wabelgiji , pili vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini  kati ya  serikali inayoongozwa na chama cha FRELIMO dhidi ya wanamgambo wa RENAMO msituni ambapo kati ya mwaka 1981 hadi 1994 vilisababisha mamilioni ya vifo katika nchi hiyo.

Ilikuwa ni Oktoba 1992 katika moyo wa Roma, kwenye  makao makuu ya Mtakatifu Egidio, ambapo walitia saini  mkataba wa kuisha vita vya wenyewe kwa wenyewe, kwa njia ya mchakato uliokuwa umeanza miaka miwili kabla. Siku hiyo ilikuwa ni ya aina yake, anakumbuka Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio Bwana Marco Impagliazzo. Sahihi hiyo ilitiwa na watu wanne Andrea Riccardi mwanzilishi wa Jumuiya, Matteo zuppi ambaye sasa ni Askofu Mkuu wa Bologna, Mario Raffaeli kutoka serikali ya Italia, Askofu wa Beira Jaime Goncalves ambao waliweza kuwakushirikisha wengine kama wapatanishi, kutoka mataifa makubwa ya Ulaya na hata mengine ya Afrika, ili waweze kuchangia kupata suluhisho. Bwana Impagliazzo anaongeza kusema,mafaniko makubwa ya suala hili ilitokana na umakini wa kutunza  siri na uwasilishaji wa mikutano hiyo kati ya wanamgambo hao  na wawakilishi wa serikali. 

Ikumbukwe historia hiyo ya msumbiji, kwa miaka mingi familia ya Mungu imekuwa ikiishi kwa hofu na mashaka kutokana na vita ya wenyewe kwa wenyewe, iliyokuwa inaendeshwa kati ya Chama tawala cha FRELIMO kilichoko madarakani na Chama cha upinzani cha RENAMO. Bwana Alfonso Dhlakama, ndiye kiongozi mkuu wa RENAMO ambaye kuanzia mwaka 1976 Msumbiji ilipojipatia uhuru wake amekuwa akiendesha vita ya wenyewe kwa wenyewe, hadi mwaka 1992, Msumbiji ilipotia sahihi kwenye Mkabata wa amani na hapo wananchi wakaanza kuwa na matumaini ya Msumbiji yenye amani. RENAMO kikageuka kuwa ni Chama cha upinzani na kuanza pilika pilika za kuwania uongozi wa nchi. Lakini hakijawahi kufanikiwa kutwaa madaraka na kuongoza nchi. 

Wachunguzi wa mambo ya kisiasa wanasema, uchu wa madaraka ulivuruga RENAMO ikakataa kukubali kushindwa kwenye chaguzi kuu za Rais na Wabunge na hatimaye, kurejea tena msituni kutaka kushika madaraka kwa njia ya mtutu wa bunduki. Kuanzia mwaka 2014 kumekuwepo na mchakato wa majadiliano na FRELIMO ili kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa,lakini ni jambo ambali hakufanikiwa kwa FRELIMO,kwani ilikazania  hasa kutaka demokrasia na utawala wa sheria kuheshimiwa na wote.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.