2017-10-02 10:14:00

Papa:Hesabu za Mungu zikoje,anazidisha maradufu akiwa anagawanya!


Baba Matakatifu Francisko aliandaliwa chakula  cha mchana kwa heshima kubwa mjini Bologna akiwa na maskini, wahamiaji na wafungwa kwenye Madhabahu ya Mtakatifu Petronio. Kabla ya chakula hicho, ametoa hotuba fupi: Ni furaha kubwa kuwaona watu wengi katika numba! Ni kama ile nyumba ya mama yetu na nyumba ya huruma ni Kanisa kwa ajili ya kuwakaribisha wote zaidi wale wenye kuwa na mahitaji ya kupata nafasi.

Baba Mtakatifu amesema kuwa,wao ndiyo kiini cha nyumba na ambayo Kanisa linawathamini kwani wao ni kitovu. Kanisa halina  nafsi nyingine tofauti na kutovu hicho na kwa pamoja. Baba Mtakatifu anaongeza, wote tumealikwa japokuwa ni kwa neema  tu! ndiyo maajabu ya upendo upeo ambao Mungu anatukirimia kama watoto wake wasio stahili upendo huo.

Aidha Baba Mtakatifu anabainisha kuwa, Kanisa lile kwa Kawaida linaadhimishwa Ekaristi, mahali ambapo wanaandaa mkate na divai ili viugeuke kuwa mwili na Damu ya Yesu katika kuwamegea na kuwanywesha watu wengi ambao Yeye mwenyewe anawapenda. Lakini maajabu ya hesabu ya Mungu ni ya kushangaza: kwa maana mkate unaongezeka mara dufu katika kugawanya. Hivyo ni lazima daima kuandaa meza ya upendo kwa wale wenye mahitaji. Upendo hauishi kamwe na huna njia moja tu, daima unazunguka wote wanatoa na kupokea chochote.

Wote tunapokea na tunatambua pia kuto sana Baba Mtakatifu anasisitiza na kuongeza; Yesu habagui yoyote, wala kudharau hata mmoja. Yeye ana kiu kuomba maji ya kunywa, Yeye anatembea na sisi na kuteseka nasi. Na ndiyo maana sisi tunayo ndoo ya kuchota maji na kutoa maji, hata kama imechakaa, lakini inaweza kutoa maji maana ni moyo wetu. Maisha yetu daima ni tunu, hivyo kila mmoja hawezi kukosa chochote cha kutoa.

Mara baada ya chakula, kila mmoja amepokea Injili, ambapo Baba Mtakatifu pia ameweza kusema maneno mafupi kuhusiana na zawadi hiyo kwamba:  pokeeni wote na iwe ni ishara na muhuri pekee wa urafiki na Mungu anayefanya hija bila kuwa na nafasi na ili aweza kuwaandalia wote makao. Wote tu wasafiri na waombaji wa upendo na matumaini. Tunahitaji huyo Mungu ambaye anajifanya kuwa karibu na wote kwa maana ya  kujionesha katika kuumega mkate.  Mkate huo ni upendo ambao leo hii umeshirikishwa  na hivyo wapelekee hata wengine, wagawie kwa furaha na urafiki.

Anaye omba mkate Baba Mtakatifu anabanisha ni kuonesha uaminifu kwa Mungu wa mahitaji yetu msingi ya maisha. Ni mara ngapi Yesu ametufundisha sala hii inayojielesha na kukusanya sauti za wale wanaoteseka na matatizo mbalimbali ya kuishi. Baba Mtakatifu amewakumbusha juu ya wafuasi wake walivyo muomba Yesu awafundishe kusali, kwamba aliwajibu kwa maneno ya kimaskini, kumwelekeza Baba wa mbingu anayetuambia kuwa sisi wote tu ndugu. Sala ya Baba yetu inajieleza kwa ujumla: utupe leo  mkate wetu ni kuomba  kwa ujumla , maana yake ni kushirikishana; kwa maana ya kushirikishana na uwajibikaji wa pamoja. Katika sala hii kila moja anatambua mahitaji na kushinda kila ahina na hitaji la dharura na kila aina ya ubinafsi ili kuweza kuchuchumalia furaha na mapokezi ya pamoja.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.