2017-10-02 10:01:00

Papa Cesena:Sera za kisiasa ziwe mstari wa mbele kusikiliza sauti za watu


Baba Mtakatifu Francisko tarehe 1 Oktoba amefanya ziara yake katika Mkoa wa Emilia Romagna. Ni  ziara aliyoianza  alfajiri mapema kutoka katika uwanja ndogo wa ndege mjini Vatican na kutua katika uwanja wa ndege wa Cesena, mahali ambapo amepokelewa na Viongozi wa Kanisa na Serikali. Viongozi hao walimwongoza  Baba Mtakatifu katika  msafara hadi  Cesena katika uwanja asubuhi uliotayarishwa kwa ujio wake. Katika uwanja huo  ametoa hotuba yake na kusema kuwa, anayo furaha kuwapo katika eneo hilo na wazalendo, kiwanja hicho  chenye kuwa na maana kubwa katika mji wao. Ni mji uliojaa uzalendo na wenye utajiri wa kihistoria ambapo kati ya wazaliwa umeweza kutoa mapapa wawili : Papa Pio VI ambaye wanakumbuka miaka 300 tangu kuzaliwa kwake pia Papa Pio VII.

Katika karne nyingi uwanja ule umekuwa ni kiini cha makutano ya wazalendo, kwa maana ndipo wanafanya soko hadi leo hii. Kwa njia hiyo inastahili kuitwa uwanja wa watu, maana rahisi uwanja, nafasi ya kijami mahali ambapo watu hutoa maamuzi, pia ndipo kuna jengo la utawala wa Wilaya. Ni mahali ambapo wanatoa maamuzi ya kiuchumi na kijamii. Ni uwanja wambao unaweza kuvuta kila mmoja katika kukabiliana na dharura, matarajio, ndoto za pamoja. Baba Mtakatifu anatoa mfano kuwa anataka kufikiria kwamba ni kama vile unga wa ngano ambao umesha tayarishwa kuokwa kwa ajili ya wema wa watu wote na kufanya kazi kwa pamoja. Ni katika uwanja huu wanachukua maamuzi ya kila siku ya kufuata katika uwajibikaji na kiakili kwa ajili ya wema wa wote. Hiyo inafanyika ili wote hata walio wadogo wanaweza kunufaika kazi na kazi, fursa za nafasi katika maisha ya raia na kuishi kwa ushirikiano.

Baba Mtakatifu anasema, kiini cha kuwapo katika uwanja huo ni kutoa ujumbe muhimu wa kufanya kazi kwa pamoja kwa ajili ya wema wa wote. Huu ni msingi wa serikali ya mji kuufanya uwe mzuri katika kukaribisha, kuanzisha hata injini ya maendeleo endelevu ya kijamii. Uwanja huo kama uwanja mwingine anasema Baba Mtakatifu, unatoa mwaliko wa maisha ya kijumuia kufanya sera za kisiasa zilizo njema. Siyo sera za kujipendelea binafsi au kwa kutumia nguvu au maslahi binafsi. Ziwe sera za kuhudumia na katika kijikita kwenye ushirikiano , baba mtakatifu anakazia kuwa  ubinafsi mwijo, bali ni kuwajibika kwa namna ya kijasiri na busara, wakati huo huo ni kutazama binadamu na maendeleo yake bila ubaguzi, kushirikisha bila kuacha wengine pembezoni.

Baba Mtakatifu Francisko anabaisha nini maana ya kufanya sera za kisiasa na mwanasiasa mzuri aweje: Siyo rahisi kuwa mwanasiasa mwema  kwasababu ili kuweza kuwa  mwanasiasa mwema , inabidi kujisadaka kwa maana ya kuweka kando mawazo yako binafsi. Siyo mawazo hayo unayaacha, bali ni kayapeleka mbele ya wengine ili kuweza kudiliana kwa pamoja  kwa ajili ya wema wa wengine. Na hizo ndiyo maaa ya kufanya sera za  kisiasa Baba Mtakatifu anasema. Kwa njia hiyo anawalika kufuata na hasa kuwa na ujasiri wa kutubu au kusema ukweli unapokosea. Huo ndiyo ubinadamu. Ametoa mifano ambayo wanaweza kutumia katika kujikosoa kwamb, wanaweza kutumia  vyombo vya habari kama radio au televisheni. Lakini la Muhimu wanao fanya siasa wawe na ujasiri wa kufanya siasa njema na kukubali kukosolewa pale inapobidi. Hiyo ni kwasababu anasema wote tunakosea maana ni binadamu , lakini kuwa na ujasiri wa kutubu ni jambo jema.

Baba Mtakatifu anawakumbusha kuwa mji huo kama Mkoa mzima wa Romagna, umekuwa na utamaduni wa hamu ya kupenda michakato ya siasa. Kwa njia hiyo anawaalika watu wote wagundue hata leo hii umuhimu wa kuishi kijamii na kutoa mchango wao na hasa wawe tayari kuonesha wema wa hayo yote. Kuwa tayari kutambua kila aina ya mawazo yenye uhakika, katika kukabiliana na hali halisi. Hiyo ni pamoja na kutazama hali halisi ya sasa, kutafuta kila njia nafasi za ajira kwa watu katika kukuza wema hadi kufikia furaha ya watu. Wawasikilize watu wote kwa maana watu  wote wana haki ya kusikilizwa sauti zao,  hasa vijana na wazee. Vijana wana nguvu ya kuepeleka mbele mambo mengi na wazee kwa sababu wanayo hekima ya maisha na madaraka juu ya vijana, hata vijana wapo katika sera za kisiasa. Wazee lazima kuwasaidia vijana mahali wanapokesea na kuwasaidia vilevile vijana pia hawana budi kutoa maoni yao kwa wazee paele inapobidi.

Baba Mtaktifu pia anaonesha wasiwasi wa sera za kisiasa leo hii na kusema, sera za kisiasa kwa miaka hii zinaonesha matendo ya mivutano, hata katika aina  nyingine zinazojikita katika utawala,  kifedha na katika mitandao. Katika hali hiyo baba mtakatifu anatoa wito wa kufanya siasa nzuri, yenye haki, uhuru wake , uwezo wake  wa kuhudumia wema wa umma na kufanya matendo ya utetezi wa wale wasio kuwa na haki sawa, wanakosa usawa wa haki za jamii, kukuza jamii ya famiia kwa hatua thabiti, kutoa mfumo imara wa haki na usawa wawote. Na mwisho anasema, kwa wale wote wanaojitambua katika matinki hii ya kisiasa na utamaduni basi wafanye siasa iliyo nzuri , ambayo iko mstari wa mbele katika utetezi na kuleta maendeleo  endelevu ya binadamu.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.