2017-09-30 15:55:00

Misa ya Sikukuu ya Malaika Michaeli msimamizi wa Vikosi vya Ulinzi Vatican


Katika maadhimisho a Sikukuu ya malaika wakuu, hata Kikosii cha walinzi Mjini Vatican, wameadhisha Sikukuu ya somo wao ambaye ni Malaika Mkuu Michaeli. Misa hiyo imeongozwa na Kardinali Pietro Parolini, Katibu wa Vatican.  Katika mahubiri yake, hawali ya yote anawashukuru  viongozi wakuu wote wa walinzi wa Vatican, pia waziri wa Ulinzi wa ndani ya nchini Italia alieyeongozana na  Wakuu wa Polisi wote kutoka nchini Italia kushiriki Misa hiyo katika kusheherekea Sikukuu ya Malaika walinzi kwa namna ya pekee somo wao Malaika Michaeli.

Kardinali pia anasema kuwa kwa  niaba ya Baba Mtakatifu anawashukuru Vikosi vyote vya Vatican kwa ajili ya huduma yao ambayo wanaitoa katika mji wa Vatican. Utume walio wao na  uwepo wao, umakini, ukarimu na upole katika kufuata sheri muhimu na maalumu katika maandilizi, ni mfano borawa hali ya juu kimaadili. Kardinalii Parolin anaongeza, iwapo katika shughuli zote inasimika mizizi ya imani na kupenyeza katika akili na moyo inatoa nguvu ya uhakika na utulivu kwa shughuli na mafanikio mema ya kazi yao.

Kardinali anabainsha  kuwa huo ni mfano  bora wa ushirikiano mzuri wanao uendeleza kati yao na ambao ni nyeti  kwa ajili ya mafanikio ya utume wao, kwa njia hiyo anatumaini  kuwa unaweza kupata faida zaidi na zaidi  kutoka kwa kila mmoja kwa njia ya kubadilishana faida nyingi za  uzoefu wao  na habari. Kujikita zaidi katika kumtambua Mungu, ndiyo nguzo kubwa katika  ufanisi kwa maana ya kuwa na hofu ya Mungu ambayo inawasidia kutojiachilia katika kutawaliwa na ulaghai wa kufuata kwanza kukidhi haja binafsi,  lakini  baadaye ndiyo matokeo ya kuleta vurugu na mabaya yanayopelekea njia ya upotofu.

Kwa njia hiyo anawahimiza zaidi kuwa na mahusiano  karibu na Bwana. Tendo la kuwa na uhusiano na Bwana ni kuhepusha kwa maana yakuhepusha hali ya kuwa  mbinafsi, kujipendelea,kuwa karibu na Bwana inakupa uwezo wa  kukaribia jirani, zaidi ni kugeuka kwa namna ya pekee kuwa na uwezo  wa kujisadaka kwa ajili ya furaha ya wengine, kwa ajili ya wema wa Jumuiya ya Kanisa na jamii pia. Kardinali anabainisha njia ya kuweza kufikia kujisadaka ni kujikita  kwa undani zaidi katika sala na utambuzi wa Mungu kwa matumaini, kwa njia ya  mabombezi ya Mtakatifu Malaika Mkuu Michaeli somo wao.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.