2017-09-30 15:24:00

Balozi Joseph Kojo Akudibillah awasilisha hati za utambulisho Vatican


Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa, tarehe 29 Septemba 2017 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mheshimiwa Joseph Kojo Akudibillah, Balozi mpya wa Ghana, mjini Vatican. Itakumbukwa kwamba, Balozi Joseph Kojo Akudibillah alizaliwa tarehe 21 januari 1948 huko Konongo-Odumasi. Ameoa na amebarikiwa kupata watoto wanne.

Balozi Kojo, kitaaluma ni muuguzi ambaye katika maisha yake, alifanikiwa kutekeleza dhamana na wajibu wake kwenye katika sekta ya afya tangu mwaka 1978 hadi mwaka 2000 katika nyadhifa mbali mbali hadi kuteuliwa kuwa waziri wa afya nchini Ghana kuanzia mwaka 1998 - hadi mwaka 1999. Alishawahi kuwa mbunge tangu mwaka 2001 hadi mwaka 2004. Mwanachama wa ECOWAS; Naibu waziri wa ulinzi na usalama na hatimaye, Mkurugenzi mkuu wa Hospitali ya Kropo Chairty ya Kumasi, Ghana, kazi aliyoitekeleza kuanzia mwaka 2004 hadi alipoteuliwa kuwa Balozi wa Ghana mjini Vatican.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.