2017-09-29 17:06:00

Papa:Mwaka wa huruma ni kipindi cha neema katika uinjilishaji wa watu


Baba Mtakatifu ametoa hotuba yake kwa wajumbe wa Mkutano wa Mwaka wa Baraza la kipapa kwa uhamasishajiwa Uinjilishaji mpya. Baba Mtakatifu katika hotuba yake anafurahi kutafakari  juu ya dharura ya Kanisa , kwa namna ya pekee katika kipindi cha kihistoria, na kurudia kwa upya nguvu katika kuimarisha utume wa uinjilishaji . Anamshukuru Kardinali Fisichela  Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Uinjilishi kwa maneno hotuba yake, na  wajibu wake katika shughuli za kujiendela katika Jumuiya ya Kanisa iweza kuwa na matunda ya jubileo ya huruma.

Mwaka huu umekuwa ni kipindi cha neema ambapo Kanisa zima limefanya uzoezo wa imani na kiroho.  Kwa njia hiyo haiwezekani, kutokufikiria au kuisahau matendo ya huruma , Baba Mtakatifu anasema. Waamini wamesikia  na kuonja kwa nguvu zote  zawadi ya huruma  na kuishi Jubileo ambayo imewafanya kugundua kwa namna ya pekee ile sakramenti ya kitubio. Ni fursa pekee ya kufanya uzoefu wa ukarimu, upendo wa  Mungu kwa msamaha wake usio na kikomo.Ni wazi kabisa kutambua jìnsi gani ya tukio la wokovu linaweza kuwa na maana kamili katika maisha ya binadamu na jamii.

Kutangaza huruma ni hali halisi inayoonekana kwa namana ya pekee katika  maisha ya kila mwamini , kuishi na kufanya matendo mengi ambayo ni wajibu wa kila anaye injilishwa , aliyegundua wa kwa mara ya kwanza wito wa kitume na nguvu ya huruma. Maneno ya Mtakaifu Paulo,  daima yasisahulike kwa wale wote wanajikita katika kutangaza Injili. Akisema kuwa anamshukuru yule anaye mpatia nguvu Bwana Yesu Kristo,  (1 Tm 1,12-16).
Katika kuelezea juu ya uinjilishaji , Baba Mtakatifu Francisko anasema, ni lazima kugundua daima asili ya watu wa Mungu. Anasisitiza juu ya mambo mawili,  kwanza, uhusiano wa kila watu kutegemea na tamaduni  zake kwenye safari ya watu wa Mungu. Baba Mtakatifu anafafanua, kila watu mahali ambapo sisi tunaelekea, upo utajiri ambao Kanisa linaalikwa kuutambua na kutoa thamani ili kuweza kufikia ukamilifu wa umoja , ambao ni ishara ya sakramenti.

Na umoja huo unaundwa kwa mujibu wa mwili lakini pia hata roho inayoongaza hatua zetu. Utajiri unaotokana na Kanisa na tamaduni za kila watu walizo nazo ni thamani ya kuishi katika matendo , hasa katika kufungua mioyo na  kupokea habari njema ya Injili.  Hizo ndiyo zawadi za kweli ambazo zinaeleza ukweli usio na  kikimo katika matendo ya  uumbaji wa Baba katika umoja wa Kanisa linaloitwa kuhudumia kila mahali , na kwa mazungumzo ya dhati.
Watu walionjilishwa wanakuwa na utambuzi kwamba ni wito utokao kwa Mungu,  kila anayekubali kuingia katika mahusiano hayo na Mungu, umwezesha aweze kufanya uzoefu wa kina wa umoja na binadamu katika jumuiya ya waamini. Baba Mtakatifu Francisko anaongeza, hiyo ndiyo inayohitajika katika nyakati zetu kwa namna ya pekee.

Ni muhimu kutambua namna ya kuijilisha katika mioyo ya watu , ili kuweza kugundua ila maana ya upendo wake anao utoa kwa imani na matumaini. Kutazama mbele kwa utulivu , pamoja na matatizo ya umasikini ambao  wanawafanya watu waishi kwa kile kidogo walicho nacho.  Baba Mtakatifu anasema , Kanisa bado lina uwezo wa kutazama kwa kina , na wanaweza kutafuta bado yale matashi ya Mungu ambaye anatuliza mioyo ya wengi walio anguka katika utotafauti, wasio weza kujenga maisha yao ya baadaye. Na furaha ya Injili inaweza kabisa kuwafikia wengi na kuwajenga wao nguvu katika mioyo ya uongofu.

Baba Mtakatifu anamalizia, uinjilishiji mpya ambao sisi tinaalikwa kufanya ni ule wa matendo ya dhati kwa upande wa Kanisa zima linalosafiri kueleka kwa Mungu. Ni lazima kugundua upeo huo wenye maana katika hatua za kichungaji  ili kuweza kusaidia uinjilishaji wenyewe, bila kusahau thamani ya kijamii ambayo ni nyeti katika kuamasisha maisha ya binadamu kamili.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.