Wito wa Malaika na sisi ni sawa, kwa kushirikiana pamoja katika mpango wa ukombozi
wa Mungu, na hiyo imeandikwa katika maombi ya siku ya leo . Ni maneno ya Baba Mtakatifu
Francisko katika mahubiri yake kwenye Kanisa la Mtakatifu Marta wakati wa tukio la
Sikukuu ya Watakatifu Malaika Wakuu Michaeli, Rafaeli ina Gabrieli.
Baba Mtakatifu Francisko anasema, tunaweza kusema kuwa sisi ni ndugu katika vito.
Wao wako mbele ya Bwana wakitoa hudima , wakisisifu na kutakafari utukufu wa Bwana
na hivyo Malaika ni wakubwa katika kutafakari.Hata hivyo Bwana anawatuma kutusindikia
katika safari yetu ya maisha.
Baba Mtakatifu akilezea uwajibu wa kila malaika anasema, Malaika wakuu watatu wanao
wajibu wao katika safari yetu ya wokovu kwa mfano Malaika Michaeli anapambana katika
vita na shetani, ambaye ni joka kuu la kizamani ambalo linasumbua daima maisha yetu,
linakaa ardhi hii kama lilvyo mdanganya mdanganya mama yetu Eva na baada ya kuanguka
likamuhukumu mbele ya Mungu.
Kwa kutumia maneno ya ulaghai, kula tunda kwa maana utatambua mema na mabaya na mambo
mengi. Yeye ni mdanyanyifu , kwa maana shetani anatumia ulaghai na ndiyo maana anasema
mdhambi ni wangu. Anatumia ulaghai, lakini Mungu anamtuma Malaika Michaeli kupambana
naye katikavita. Bwana alimwomba afanye vita na shetani huyo kwa ajili yetu sisi tuliyo
katika safari kuelekea mbinguni. Malaika Mikaeli anatusaidia kupambana katika vita
na hatuachi kwamwe tuingie katika ulaghai.
Malaika Michaeli anayo kazi ya kulinda Kanisa na kila mmoja, tofauti na kazi ya Malaika
Gabrieli ambaye ni mpeleka habari njema. Yeye alipeleka habari njema na ya wokovu
Kwa Maria, Zakaria na Yosefu. Hata Malaika Gabrieli daima yuko nasi , anathibitisha
Baba Mtakatifu, anatusaidia katika safari yetu na hasa tunaposahau Injili ambayo
ni Yeu amekuja kwa ajili ya kutukomboa.
Malaika wa tatu, Baba Mtakatifu anaeleza, Rafaeli, ambaye anatembea na sisi na ili
tusielekee katika njia potofu. Kwa njia hiyo wasindikizaji wetu katika huduma ya
Mungu na maisha yetu , wanatufundisha leo hii kusali kwa njia rahisi, kama vile ,
Michaeli atufundishe kupamba na kila mmoja atambue namna ya kupamba na maisha yake
kuondokana na ubaya wa shetani mwovu. Malaika Gabarieli atusaidie kupeleka habari
njema ya wokovu kwa kuwatangazia wote kuwa yeye anaishi na tupo pamoja naye katika
safari ya kuelekea kwa Baba yake.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |