2017-09-28 17:18:00

Papa ametuma ujumbe katika Mkutano Mkuu Baraza la Maaskofu Ulaya


Tarehe 28 Septemba 2017, Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe wake katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Baraza  la Maasko wa Ulaya (CCEE), uliotiwa saini ya Kardinali Pietro Parolin Katibu Mkuu wa Vatican. Baba Mtakatifu anatoa salam zake kwa washiriki wote wa Mkutano huo wa mwaka akiwatia moyo waendelee na shughuli hiyo muhimu ya kuweza kung’amua njia za kupitia katika kushirikiana kwenye shughuli za kichungaji katika nchi mbalimbali na wakithamanisha utofauti na kuhamasisha vitendo vya kuanzisha  mshikamano wa kindugu.

Baba Mtakatifu anawatakia Mkutano Mkuu uwe fursa ya kuchangia na kuimarisha mahusiano yaa umoja na muungano kati ya maaskofu wa Ulaya, kwa kujiita ndani zaidi na kwa ujasiri katika utume wa Kanisa la Ulaya, hasa katika kuwaimarisha vijana,  kuwasaidie wawe na mang’amuzi kwenye  mwanga wa imani na miito yao katika jumuiya ya kikristo na katika jamii. Katika hisia hizo anawaomba kwa moyo wa dhati wadumu katika sala kwa ajili yake; anawatumia baraka za kitume.

Kuhusiana na Mkutano huo , taarifa zinaonesha kuwa, ni kwa mara ya kwanza katika historia ya Mkutano wa Nwaka wa  Baraza la Maaskofu wa Ulaya kufanyika huo  Bielourusi ili kukutana na jumuiya Katoliki mahalia na kuadhimisha miaka 750  ya kutangazwa kwa mji wa Minskna  maadhimisho ya miaka 500 ya kuchapisha Biblia katika lugha ya Bielourusi.

Kwenye Mkutano  wa mwaka watakabiliana na mada juu ya vijana, kwa namna ya pekee kuona sura ya kijana leo hii, shahuku  zake, mahitaji yake , hofu zake, matarajio, uhusiano wake. Halikadhalika changamoto za dunia hii ambazo zinaendelea kujitokeza katika Kanisa na kufikiria namna mpya ya kujikita katika njia za  Kichungaji. Watatoa mapendekezo ya Injili kwa namna ya pekee kwa watu wambao wanaunda Kanisa la kesho.
Maada ya pili katika Mkutano wao  itakuwa ni kuhusu Bara la Ulaya , kwa namna ya peke mchango na utume wa Kanisa katika ujenzi wa nyumba ya pamoja. Huko Minsk, Wenyeviti wa Mabaraza ya maaskofu wa Ulaya watajadiliana kwa pamoja namna gani ya kutangaza Injili ya Kristo katika Bara la Ulaya.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.