2017-09-28 16:37:00

Hotuba ya Ask.Mkuu Auza kwa Siku ya Kimataifa ya kudhibiti silaha za nyuklia


Kudhibiti moja kwa moja silaha za kinyukilia ndiyo lengo msingi katika maendeleo ya kweli ya dunia, kwa mtazamo wa amani ya kizazi kipya na  katika maendeleo endelevu.  Ndiyo imekuwa hoja ya  hotuba ya Askofu Mkuu Bernardito Auza Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Ofisi za umoja wa Mataifa mjini New York  tarehe 26 Septemba 2017 katika tukio la Siku ya Kimataifa ya kuthibiti moja kwa moja  silaha za kinyuklia iliyozinduliwa tangu mwaka 2013 .

Mkutano wa ngazi ya juu uliofanyika siku zilizo pita baada ya ufunguzi wa kutia saini katika Mkataba wa kuthibiti silaha za nyukilia uliofanyika terehe 20 Septemba 2017. Saini za Mkutana huo zilianza  tarehe 7 Julai 2017 na kusainiwa na nchi 150 .
Katika hotuba yake,  Askofu Mkuu Auza anasema Vatican, imetia saini ya mkataba huo wa kuthibiti silaha za nyuklia ili mkataba huo uweze kuleta  matumaini kwa wale watu wanaoishi na wale ambao bado watazaliwa kila siku katika sayari hii ambayo inaweza kuwa huru kutondokana na silaha. Ni karibu miaka 70 sasa inaendelea kuleta vizingiti na matarajio ya binadamu katika amani. 

Askofu Mkuu Auza aidha amekumbusha ujumbe wa Baba Mtakatifu katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa mwezi machi. Katika tukio hiloBaba Mtakatifu anasisitiza kuwa,  amani ya kudumu ya kimataifa haiwezi kusimamia juu ya mtazamo wa usalama wa uhongo au katika vitisho na uharibifu wa pamoja au mivutano. Amani lazima  kujengwa juu ya haki, maendeleo kamili ya binadamu, heshima na haki msingi za binadamu, ulinzi wa mazingira , ushiriki wa wote katika maisha ya umma, uaminifu kati ya watu, kuhamasisha katiba za amani na kushiriki kwa wote katika elimu na afya.

Askofu Mkuu aidha  anabainisha muhimu kushinda mitazamo rahisi ya kuzuia nyuklia na kupitisha mbinu  mbalimbali za kudumu . Hata hivyo, kuna vyombo vya kisheria. Mkataba wa kuzuia Silaha za Nyuklia kwa sasa  ki ukweli umeongeza ile mikataba mingine miwili. Ya kwanza ni Mkataba wa kudhibiti Silaha za Nyuklia, uliofunguliwa kwa saini mwaka wa 1968 na ulianza kutumika tarehe 5 Machi 1970. Katika Mkataba huu hata hivyo mapema wiki hii  Baba Mtakatufu katika tweet yake amesema "Hebu tujibidishe  katika  ulimwengu bila silaha za nyuklia, kwa kutumia Mkataba wa kukomesha vyombo hivyo vya kuleta kifo”. Mkataba huo ulisainiwa na nchi  191, ikiwa ni pamoja na Vatican ambayo iliidhinisha tangu 25 Februari 1971. Nchi pekee ambazo hazikubali kuingia ni India, Israeli na Pakistan. Korea ya Kaskazini iliondoka  katika makubaliano mwaka 2003.

Chombo cha pili cha kisheria cha kimataifa ni Mkataba  wa Kimataifa wa uzuiaji wa Majaribio ya Nyuklia uliofunguliwa kwa saini tarehe 24 Septemba 1996 na ukaweza ktumika rasmi kwa siku 180 baada ya kuthibitishwa na mataifa 44 yenye mitambo ya nyuklia, iwe ya kijeshi au ya kiraia (haya majimbo yameorodheshwa katika Kiambatisho cha  II cha Mkataba).
Kwa sasa, majimbo yaliyothibitishwa ni 166, ikiwa ni pamoja na Vatican, ambayo ilijiunga 18 Julai, 2001. Lakini bado nchi 8 kati ya 33 wenye vituo vya kinyuklia nchi hizo ni : Marekani, China, Korea ya Kaskazini, Misri, India, Iran, Israeli na Pakistan na bila kuthibitishwa kwa nchi hizi, Mkataba hauwezi kuwa kamili.

Vyombo  tatu vya kisheria vinasaidia kwa nguvu   na hufanya mtandao muhimu wa vigezo na viwango ili kuhakikisha ulimwengu unaondokana na hatari hiyo na kuwa huru na silaha za nyuklia. Lengo la dharura anavyokumbusha Baba Mtakatifu Francisko katika mkutano juu ya athari za silaha za nyuklia, Desemba 2014. "Silaha za nyuklia ni shida ya kimataifa inayoathiri  mataifa yote na kutakuwa na athari kwa vizazi vijavyo, kama vile kwenye sayari ambayo ni nyumba yetu.

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.