2017-09-28 14:59:00

Askofu Mkuu Savio Hon Tai-Fai ateuliwa kuwa Balozi nchini Ugiriki


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Savio Hon Tai-Fai, kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Ugiriki. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Savio Hon Tai-Fai alikuwa ni Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu. Itambukwa kwamba, alizaliwa tarehe 21 Oktoba 1950 huko mjini Hong Kong. Baada ya masomo na majiundo yake ya kitawa katika Shirika la Wasalesian wa Don Bosco, akapewa daraja Takatifu ya Upadre, tarehe 17 Julai 1982.

Kunako tarehe 23 Desemba 2010, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Askofu mkuu na Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu na kuwekwa wakfu kama Askofu mkuu tarehe 5 Februari 2011. Ni kati ya vigogo waliojisadaka kutfasiri Katekisimu Mpya ya Kanisa Katoliki katika lugha ya kichina!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.