2017-09-26 15:52:00

Wakristo wa Kanisa Italia wanaalikwa kutoa huduma ya binadamu


Ni lazima  kuwajibika kwa dhati, katika kanisa, maaskofu, mapadre , watawa mashemasi na walei, kama vile asema vyo Baba Mtakatifu kuwa kila mmoja afanye sehemu yake , kwa maana kuna haja  wote kujikitia katika utume ili kila mmoja waweza kuwa mshiri wa kuleta ukamilifu  na umoja wa kanisa.
Ni maneno yaliyomo katika Ripoti ya Kardinali Gualtiero Bassetti Rais wa Baraza la maaskofu Nchini Italia wakati wa Mkutano wao Mkuu. Kardnalia anasema  Kanisa la Italia linapeleka mwaga wa Kristo katika dunia mpya na lazima kujikita katika thamani ya maelekezo ya mwongozo wa kanisa. Ni kushirikiana na kushirikishana hekima ya kizamani na ile ya sasa katika mafundisho ya kanisa , kwa njia ya Roho ya kimisionari, tasaufi ya umoja , na utamaduni wa upendo.

Wote wameitwa hawali ya yote kuwa katika huduma ya binadamu mwenye majeraha, na ndiyo hiyo maana ya Kanisa la Kimisionari. Utume wa kikristo ni kutangaza Injili yake kwa furaha , kusimika mzizi  ambayo inaweza kuleta mapinduzi lakini kirahisi.Ni  Kutangaza kwa furaha Injili, kama isemavyo Hati ya Furaha ya upendo kwa sababu ni muhimu na haku chochote zaidi cha dhati na dhahiri zaidi ya Injili. Kardnaiali Basseti anasema hiyo ndiyo  upeo wa kifranciskan ambao kila mmoja anapaswa kuwa nao na kujikita kwa kina zaidi katika hali ya sasa ya kanisa. Kuna mahitaji  makubwa katika utume wa uinjilishi ndani ya mvutano  na uwezo wa maeneo yaliyo mengui ya kisasa.Ni kuhakikisha ya kwanza shughuli za umisionari kichungaji  zinakuwa mstari wa mbele na  ndiyo maana Mtakatifu Paulo anasema, ole wangu  mimi nisipo tangaza  Injili, na ndiyo upeo na ndoto ya kimisionari ya kupeleka mbele kwa watu wa Mungu. Anasisitiza Kardinali Bassetti.

Halikadhaliaka akieleza  juu ya tasaufi ya umoja, anasema mojawapo ya mtendo mema ya Kanisa la Italia , ni ule umoja ikiwa ni matunda ya kihistoria  na mizizi ya kijasiri ambayo imedumu katika kuanzisha mamno mengi ya kiimani.Lakini pamoja na hayo  zipo changamoto za kisasa, ambazo zinaleta harii ya kila mmoja kuweza  kwenda vya kivyake katika njia yake. Kijibagua ni mtindo ambao unaweza sasa kuingia katika Kanisa, kwa njia inapeleka mbali kanisa  na maamuzi. Anafafanua kwamba  mwili unaishi , iwapo kila kiungo kinafanya kazi kwa pamoja.  Haiwezekani katika Mwili kuishi peke yake, kwa njia hiyo, Kardinali Basetti anawatakiwa mafanikio  ya Kanisa la Italia kubaki kitu kimoja kama mwili mmoja usiogawanyika kwa kila hali.

Aidha ameelezea juu ya utamaduni wa upendo ambao anasema, ni maisha ambayo inakwenda kinyume na hofu na ubaguzi. Nji hiyo ni mfano unaopatika katika Injili  ya msamamria mwema  na kama alivyosema Mwenyeheri Papa Paulo wa VI wakati wa kumaliza Mtaguso wa II wa Vatican Kuwa Kanisa linafanana na Msamaria. Kanisa linaalikwa kuhamasisha utamaduni wa upendo kwa ajili ya maisha ya maskini katika jamii. Hiyo ni kutokana kwamba siyo kupenda kwa maneno tu bali kwa vitendo, kama vile Baba Mtakatifu Francisko ambaye amezindua  siku ya maskini itakayofanyika kila tarehe 19 Novemba. Mbele ya macho ya masikini, Kanisa la Italia linaiga mfano wa Mtakatifu Francisko wa Assisi aliyekuwa jemedali , lakini ndani ya moyo wake ni masikini, maana alipokutana na fukara  alivua vazi lake na kumvalisha.

Maskini hata kama hawapigi kelele lakini ukikutana nao, ni sura ya Kristo. Heri masikini maana ufalme wa mbingu …Kanisa linahitaji kwenda mbio kwa maskini, ndiyo shughuli yeke ya kitume katika kuimarisha imani na namna ya kuishi katika Kanisa. Kardinali Bassetti pa anatazama kKnisa la Italia ya kwamba linahitaji kufanya mang’amuzi kwa kwa upande  vijana, familia, na wahamiaji.
Leo hii hali halisi ya ajira ni muhimu katika nchi, na hasa kwa upande wa vijana , wakati huo huo ni dharura. Pamoja na kwamba serikali inatafuta kila njia namna ya kukidhi haja  nafasi za kazi kwa ajili ya uchumi, lakini bado haiwezi kukidhi haja hiyo yote mbele ya milioni nane ya watu maskini waliojiandikisha wakisubiri ajira. Lakini wakati huo huo nusu yake hawajuhi waishije. Hawa ni familia vijana na wenye umri kati ya miaka 50, ni umri ndogo lakini wamepoteza kazi na kubaguliwa na mfumo wa siasa na kiuchumi.

Kwa njia hiyo ni lazima kufikiria kwa makini suala hili pamoja  na kutazama utume wa Kanisa katika mantiki zote. Mbele ya kipeo hiki, vijana wengi wanahitaji msaada wa neema ya mungu. Hiyo ni pamoja na Kanisa la Italia kuitwa kwa njia ya pekee kuwa karibu sana na familia. Familia nyingi katika jamii ya Italia inazidi kuongezeka matatizo ya ndani kma vile , watu wasio funga ndoa, mafarakano na ndoa kuharibika , ukosefu wa watoto ndani ya familia, ambao unazidi kutishia taifa na upungufu wa maadili pia ndani ya familia. Kwa njia hiyo Kanisa la Italia linapaswa kujikita kwaupya  katika kutafuta njia  zozote za kuingilia kati kwenye maèungufu na udhaifu wa familia, s itu bali kwa ujumla katika maisha ya kibinadamu.

Zipo aina tatu za changamoto zinazokabilia familia ya Italia lakini pia ni pamoja na Kanisa lenyewe.Kardinalia anasema, hawali ya yote  namna ya kuishi na matatizo ya ya familia kwa maana, mara nyingi kuna wasiwasi wa kutoa matunda katika familia ambayo inaundwa na  mwanaume na mke, lakini sasa  wanaishi  kama vile ni kutumia na kutupa, bila kujali maisha. Changamoto ya pili ni ile ya  kijamii ambayo haijali kipimo cha familia katika jamii. Aina hiyo inasabaishwa na ukosefu wa ajira ndani ya familia ambapo  ndani ya familia  wanaishi bila kuwa na msimamo, ndiyo unakuta watu wanachanganyikiwa na kukosa  mahusiano mema kati ya ndugu wote.

Changamoto ya tatu ni ile ya ambayo ni mada ya dharua ya sasa katika miaka 10 ya mwisho hasa inayohusu ulinzi  na thamani ya familia kati ya mume na mke amabao wanaundwa ili kufungulia maisha; imetokana zaidi na changamoto ya utamaduni  na kiroho katika nyakati zetu.
Mwisho ameongelea juu suala la wahamiaji , Kardinali anasisitiza juu ya kuwalinda , kuhamasisha na kushirikisha ya kwamba imekuwa inatekelezwa kwa dhati katika Kanisa la Italia.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.