2017-09-26 15:44:00

Papa:Familia ya Yesu ni wale wote wamzungukao kusikiliza Neno lake


Baba Mtakatifu anatafakari neno la familia ya Mungu na Yesu kuwa ni jambo muhimu ukifikiria jinsi ilivyotumiwa   na mitume na marafiki, lakini siyo tabia ya kawaida au kusema ya kuelimika  au ya kidiplomasia, kwa njia hiyo je maana ya neno hilo katika tasaufi ya mababa wa Kanisa inatufundisha nini?. Wale wanao sikiliza Neno la  Mungu na kuliweka katika matendo, ndiyo dhana  ya familia ya Yesu, familia ambayo ni pana, inayoishi katika dunia. 
Ni mananeo ya Baba Mtakatifu asubuhi ya tarehe 26 Septemba wakati wa Misa takatifu kwenye Kanisa dogo la Mtakatifu Marta mjini Vatican akitafakari Injili ya siku, ambayo Yesu alitamka wazi wakati anatafutwa kuwa, tazama, wanaosikiliza Neno ndiyo familia yake.

 Katika Injili ya Mtakatifu Luka inaonesha kuwa: Bwana anaita  mama yake,  ndugu na familia  na wale wote ambao wamemzunguka na kusikiliza mahubiri yake.  Baba Mtakatifu anaendelea, hiyo inakufanya usikilize dhana  ya familia ya Mungu na Yesu , ambaye kwa sasa anailezea nini maana yake. Baba Mtakatifu Francisko anasema, Yesu anataka utambue kuingia katika nyumba yake na kukaa, kuona mazingira yake na kuishi naye. Kuishi pale  maana yake ni  kutafakari na kuwa huru mahali hapo. Hiyo ina maana ya kwamba watoto daima wako huru hasa wale  wanaoishi katika nyumba ya Bwana, wote ni huru wanaoishi ndani ya familia ya Bwana, anasisitiza.

Wengine kwa kutumia neno la Biblia ni watoto wa watumwa, ndiyo maana wakristo wengine hawakudiriki kukaribia, hawakujua kutengeza familia na Bwana, ndiyo maana kuna nafasi kubwa inayo watengenisha na Bwana. Kama  vile wanavyofundisha watakatifu wakuu, Baba Mtakatifu naongeza, familia ya Yesu maana yake ni kukaa naye, kumtazama, kusikiliza Neno lake, kumtafuta na kufanya mazoezi na kuzungumza naye. Neno ni sala, Baba Mtakatifu anasisitiza, ambapo sala inaongoza njia katika kutafakari  na  kujiuliza je Bwana anafikiria nini, je hiyo ndiyo familia daima?. Hiyo ndiyo  njia  iliyokuwa ikifanyika na watakatifu walio wengi kwa mfano wa Mtakatifu Teresa wa mtoto Yesu alikuwa akimkuta Bwana mahali popote na kuwa familia , mfano katika kuosha vyombo, jikoni na mambo mengine aliyokuwa akifanya na kuona, Baba Mtakatifu anasisitiza.

Kuwa familia maana yake  ni kubaki katika uwepo wa Yesu, kama vile yeye anavyotushauri, katika sala yake wakati wa Karamu yake ya Mwisho. Au tunaona maelekezo zaidi  katika mwanzo wa Injili Yohane anaonesha kuwa huyo ndiyo mwanakondoo wa Mungu aondoaye dhambi za dunia. Andrea na Yohane walikwenda nyuma yake na siku nzima walibaki na Bwana. Baba Mtakatifu kwa mara nyingine anasema watu wakati mwingine mwendo wa kifamilia kwa wakaristo haukuwa mzuri, hiyo ni kwasababu walikuwa wakijitenga na kuwa mbali na Yesu. Kwa njia hiyo, Baba Mtakatifu anachukua fursa ya kuuliza iwapo kuna uwezekano wa kutoa fursa ya kuwa na tabia ya mwenendo wa familia na Bwana. Kwa mfano mkristo mwenye matatizo ambaye anakwenda kwenye Bus au Metro akiwa anaongea juu ya Bwana na anatambua kuwa Bwana anamtazama, na kuwa karibu:  hiyo ndiyo familia, ndiyo ukarimu, ndiyo kujisikia ukaribu wa familia ya Yesu.  Baba Mtakatifu anamaliza akiomba neema  kwa ajili ya wote ili kuweza kujua maana ya familia ya Bwana na Bwana atukirimie neema hiyo ya kuingia katika nyumba yake na kuwa familia moja.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya kiswahili ya Radio  Vatican.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.