2017-09-25 16:39:00

Papa amekutana na wanachama wafadhili wa walinzi wa Uswiss wa Vatican


Jumatatu 25 Septemba 2017 Baba Mtakatifu Francisko, amekutana na kuzungumza na Wajumbe wa Chma cha wafadhili wa  Walinzi wa Papa kutoka  Uswiss. Baba Mtakatifu Francisko amewasalimia kwa furaha kubwa wanachama wa sehemu zote mbili ziliundwa kwa ajili ya kuwasaidia kiuchumi, vifaa na utaalamu wa Walinzi wa Papa kutoka Uswiss, na Shukrani za pekee kwa Mwenyekiti wao Jean Pierre Roth na Pascal Couchepin, kwa maneno ya hotuba yao. Wamefika kwa ajili ya tukio la kuanzishwa rasmi kituo kipya cha shughuli zao. 

Aidha anasema kuwa anao utambuzi wa uwepo wao wakiwa pia  wanaadhimisha mwaka wa 600  wa somo wao Mtakatifu Nicola wa Flüe. Zaidi kuwashukuru kwa ukarimu wao wa  kifadhili cha Walinzi wa Uswiss,kwa ushirikiano wao na mamlaka ya Vatican.
Katika shughuli zao, wanajieleza katika roho ya umoja na mshikamano kutokana na hotuba ya Mwenyekiti wa chama, Couchepin kama vile uwepo wa wakatoliki katika chama hicho. Baba Mtakatifu anasema  mfano huo unapata mizizi na wito wa Injili ya upendo kwa ndugu, katika kuhamasisha na kushinda utofauti,  na mivutano ya kijamii katika makundi. Kwa njia hiyo wakati wa shughuli zao, wanashuhudia kwa dhati mawazo ya kiinjili ambayo ni msingi wa nchi ya Uswiss , anaongeza Baba Mtakatifu kuwa wao ni mfano wa ndugu na kushirikishana.

Upendo wa ndugu unafanana utume wa Yesu Kristo ambap unajisimika miziz yake ki ukweli katika upendo wa Mungu. Na kwa namna hiyo inawezekana Mkristo kujitoa kutokana na kwamba mizizi inatokana na Mungu mwenyewe ukarimu na upendo mkubwa. Kutoa upendo kwa ndugu, inahitaji kuchota kutoka katika moto wa upendo wa Mungu, kwa njia ya sala, kusikiliza Neno la Mungu, na kumwilishwa katika Ekaristi takatifuHivyo vyote vinajileleza kutokana na huduma yao wanayo itoa kwa Walinzi hao wa Uswiss.

Baba Mtakatifu Francisko anawashukuru kwa yote wanayotenda kwa ajili ya vijana wa Uswis wanaojitoa kwa miaka mingi kuendelea na huduma ya Kanisa na Vatican. Hii ni fursa ya pekee ambayo kwa uwepo wao wa kitalaamu na ukarimu ambao unathaminiwa Vatican. Bikira Maria na Mtakatifu Nicola Flüe awalinde na família zao wawe mashuhuda wa imani na upendo na waendelee katika wema huo wa kujitoka katika shughuli za Walinzi wa Papa.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.