2017-09-25 16:22:00

Faraja ni kama Injini ya kusukuma matumaini kwenda mbele katika maisha


Ni kuomba Bwana ili aliweze kutufundisha mvuto wa ukombozi. Ndiyo sala ya Baba Mtakatifu Francisko aliyoitoa  wakati wa mahubiri yake asubuhi ya tarehe 25 Septemba 2017 wakati wa misa Takatifu kwenye Kikanisa cha Mtakatifu Martha Mjini Vatican. Katika tafakari kutoka katika somo la siku , Baba Mtakatifu anasimulia kipindi cha Waisraeli walipo pata uhuru kutoka utumwani. Bwana aliwatembelea watu wake na kuwarudisha Yerusalem. Neno kutembelea Baba Mtakatifu anafafanua, ni umuhimu katika historia ya ukombozi kwasababu kila aina ya kukombolewa na kila tendo la ukombozi wa Mungu ni kutembelewa.

Bwana anapotutembelea anatupatia furaha. kwa maana ya kwamba anatupatia faraja, hiyo ndiyo maana ya kuvuna kwa furaha. Ndiyo walipanda kwa machozi, lakini sasa Bwana anatuliza  watu wake kiroho. Faraja hiyo halikuwa ya wakati ule tu bali ni hatua ya maisha ya kiroho ya kila mkristo, na Biblia nzima inafundisha hilo, Baba Mtakatifu anasisitiza. Aidha anatoa wito, kuwa na subira ya kutembelewa na Mungu kila mmoja, kwani katika maisha ya binadamu, kuna kupindi ambacho ni kigumu na kile chenye nguvu, lakini Bwana daima anaonesha uwepo wake na kutoa faraja ili kutujaza furaha ya kweli.

Inahitajika kuwa na subira ya tukio hilo kwa unyenyenyekevu kama vile matumaini ambayo daima ni kidogo lakini wakati mwingine ni yenye nguvu  kwani mara nyingi yanafichika ndani kama vile moto chini ya majivu Baba Mtakatifu anathibitisha.  Hivyo Mkristo anayeshi na hamu ya kukutana na Mungu, anavutwa na faraja ambayo inapatikana  wakati wa kukutana na Bwana. Iwapo Mkristo hana mvuto huo au hamu ya  kuelekea katika makutano hayo, Baba Mtakatifu anaongeza, huyo ni mkristo aliyefungwa amewekwa pembeni katika maisha, hata haelewi afanye nini katika maisha yake. Ni mwaliko kwa wote  kuwa na utambuzi wa  faraja kwasababu kuna manabii wa uhongo ambao wanajifanya kufariji na kumbe siyo kufariji , maana faraja siyo furaha ambayo unaweza kuinunua.

Faraja ya Bwana inajikita kwa ndani na kukuongezea nguvu ya upendo, imani na matumaini vilevile ni kama injini inayotoa msukumo wa kupambana na dhambi. Hata unapotazama Yesu na Mateso yake na kulia na Yesu mwenyewe. Faraja hiyo inakuza ndani ya  moyo wako kupenda  mambo ya mbinguni, mambo ya Mungu , unatuliza roho  na kuwa na amani katika Bwana, hiyo ndiyo faraja ya kweli. Baba Mtakatifu Francisko anatofautisha kati ya faraja na kujifurahisha , kwamba, faraja siyo jambo la kufurahisha tu, kwasababu hata jambo la kufurahisha siyo jambo baya, kwasababu sisi wote ni binadamu na tunahitaji kufurahia, lakini faraja ni kinyume kwasababu inajikita ndani ya uwepo Mungu na kutambua kuwa huyo ndiye Bwana.

Hali kadhalika Baba Mtakatifu  anakumbusha kumshukuru  Bwana anayepita kututembelea, ili kutusaidia twende mbele zaidi kwa kutumaini katika kubeba Msalaba. Anatoa wito wa kutunza faraja tunazopokea kwa maana ni kweli kwamba faraja ni ya nguvu, inatunzwa pia kuacha ishara zake.
Baba Mtakatifu anamalizia mahubiri juu ya faraja kwamba, ni muhimu  kutunza alama za faraja  na kutunza kumbukumbu zake, kama vile watu wa Israeli walivyotunza wakati wamekombolewa kutoka utumwani. Kwa njia hiyo hata sisi tumerudi Yerusalem maana hata Yeye aliwakomboa huko. Kusubiri faraja, kutambua faraja na kutunza faraja ndiyo njia msingi ili wakati wa kipindi kigumu uweze kubaki na amani, ambayo ndiyo hatua ya mwisho ya faraja. 

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.