Walikuwa hawataki kumruhusu kupata daraja Takatifu la Upadre, kwasababu alikuwa
mdhaifu katika taaluma, lakini baada ya kupata daraja lwa upadre, alionesha ujasiri
mkubwa na kuwa padre wa kweli katika urafiki na ndugu wote zaidi wale masikini.
Utume wake ulianzia kwa watu asili wa tzutuhil nchini Guatemala, watu ambao hawakuwa
na maisha bora, walikuwa wametengwa , hawakuwa na elimu na mambo muhimu ya kuweza
kuishi. Padre A’plas, kama alivyoitwa na watu wa asili, kwa jina la ubatizo ni Francis
Stanley Rother (1935-1981) aliyelipa maisha yake katika kujitoa kutangaza Injili kwa
watu hao.Kwa bahati mbaya mikononi mwa watu watatu wakakatisha uhai wake tarehe 28
Julai 1981 akiwa katika nyumba yake ya parokia. Kabla ya kuwawa alikwa ameshauriwa
akimbie kuacha nchi ya GUATEMALA, lakini kama mchungaji mwema alitaka kubaki na zizi
lake hadi mwisho.
Ni kutokana na ujasiri huo ambapo Kanisa Katoliki limetambua karama za utakatifu wakea na kwa njia hiyo tarehe 23 Septemba 2017 mji wa Oklahama, Marekani Kardinali Angelo Amato, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya mchakato wa watakatifu akiwakilisha Baba Mtakatifu Francisko anamtangaza Mwenye Heri Mfiadini. Historia ya mashia yake: Padre Francis Stanley Rother alizaliwa tarehe 27 Machi 1935 na Baba Franz na mama Getrude Katherine Smith katika Jumuiya Katoliki kutoka Ujerman kwenye mji wa Okarche huko Oklahoma. Alikulia katika mazingira yenye misingi mikuu ya dini Katoliki. Septemba 1953 alijiunga na Seminari ya Mtakatifu Yohane, baadaye alihamia katika Seminari ya Kupalizwa Mbinguni katika Mji wa Texas.
Baada ya kushindwa kufuzu baadhi ya masomo, Askofu Victor Reed wa Jimbo la Oklahoma na Tulsa alimpatia fursa ya pili kuendelea na masomo. Juni 1959 alitumwa kuendelae na masomo ya kiada wakati wa kiangaza kwenye Seminari ya Mkingiwa dhambi ya asili, huko Missouri ili kujiendelea kwenye lugha ya kilatini. Baadaye akatumwa tena kurudia masomo ya Taalimungu Katika Seiminari ya Emmitsburg huko Maryland. Gombera wa seminari hiyo aliweza kutambua mara moja, uwezo wake wa akili ya kawaida lakini zaidi uadilifu, juhudi zake katika maisha ya sala na kazi, kwa njia hiyo Askofu Reed akampa daraja Takatifu la upadre tarehe 25 Mei 1963.
Kwa miaka 5 ya kwanza Padre Rother alihudumia Parokia tofauti huko Durant, Tulsa na Oklahoma, akionesha kwa namna ya pekee ule uwezo wa mahusiano mazuri na jirani , hasa uwepo karibu na watu masikini na walio baguliwa. Watu walianza kuzungumzia kuwa padre huyo alikuwa mkarimu na mwema. Mwaka 1968 alipelekwa katika utume wa Jimbo la Oklahoma ambao walikuwa wamezindua huko Santiago Atitlán nchini Guatemala. Mji ulikuwa kando ya ziwa la Atitlán na maarufu kwa ajili ya uzuri wake wa asili, vilevile ulikuwa unajulikana ni mji wa watu maskini kiroho, na kimwili. Walikuwa ni watu wa asili ya tzutuhil wasio kuwa na chakula na walikuwa wanateseka na ukosefu wa elimu na magonjwa mbalimbali. Akiwa kijana padre kutoka Marekani alianza jiitihada nyingi ikiwa ni ujenzi wa Kanisa, nyumba ya mapadre, siyo hayo tu bali hata kuanza kuelimisha makatekista, na ujenzi wa kituo cha afya huko Panabaj. Vilevile alianzisha kituo cha matangazo ya radio kwa kuendesha vipindi vinavyohus mafunzo ya dini na kijamii, ambapo mpango huo wa elimu ya dini na jamii uliweza kuongeza kwa kiwango kikubwa cha maisha katika sekta ya kilimo na lishe.
Kwakuwa wakazi wengi walikuwa wanatumia lugha mbalimbali Padre Stanley, kwanza alijifunza lugha ya Kihispaniola kisha lugha ya asili ili aweze kuhubiri, kuwaongoza katika uongofu, kufundisha na kutoa sakramenti. Pamoja na wahudumu wengine katika utume wake, alianza kutafsiri Neno la Mungu la Agano jipya ili kuweza kuadhimisha misa ya kawaidi katika lugha ya asili. Katika juhudi hizo za kuwa na ukarimu na unyenyekevu watu walimpenda sana na kumpa jina la Padre A’plas. Katika eneo hili ambalo lilikuwa masikini bila kuwa na simu au zana zozote za mawasiliano, Padre Rother alifanya juhudi pia ya kuanzisha mambo mengi ikiwa ni pamoja na mafunzo ya watu mahalia na kutafuta makatekista na watu wenye uwezo wa kuendesha kituo cha radio.
Mwaka 1975 akawa paroko wa utume wa Santiago ya Atitlán na alikuwa padre mmoja tu aliyekuwapo katika parokia hiyo. Lakini wakati hu huo huo nchini Guatemala ukazuka mgogoro wa kisiasa na kuangu kwa kwa urais wa nchini Jacobo Arbenz Guzmán. Ni kipindi kilichotokea machafuko makubwa. Mwanzoni mwa 1981, padre Rother alipata taarifa kuwa jina leke lilikuwa kwenye orodha ya wale waliokuwa katika hatari ya kifo na walimshauri aondoke haraka kuacha nchi hiyo.
Pamoja na hayo alikuwa ameamua kurudi Marekani Januari 1981 na kabla kuondoka alikuwa amepata hata visa ya rafiki yake padre Pedro Bocel. Lakini Aprili 1981 Padre Rother alijisikia kutokuwa mbali na utume wake na ndipo aliamua kurudi Guatemala. Pamoja na kwamba alishauriwa kutokanyaga eneo la Santiago alijisikia kuendelea kutumikia Parokia yake kwa maana alisema mchungaji haweza kukimbia na kuwacha mifugo yake katika hatari. Tarehe 28 Julai 1981 maaskari walifika wakiwa wameziba nyuso zao waliingia katika nyumba yake na kumuua kwa risasi. Kwa namna hiyo ilitimilizika shahuku yake ya kutoa maisha yake yote hadi mwisho kwa ajili ya kutumikia Mungu kwa watu wa tzutuhil. Mwili wake ulikuwa kwanza umelazwa katika Kanisa Kuu la Mama yetu wa msaada huko Oklahoma, lakini kwa maombi ya wanaparokia wa Guatemala, masalia yake yalihamishwa katika Kanisa la Parokia ya Santiago Atitlán.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |