2017-09-20 13:58:00

Mmisionari aliyetekwa nyara nchini Mali ana matatizo kiafya


Kwa mujibu wa Polisi wa Taifa la Colombia Sr Gloria Cecilia Narvaez , mwanashirika wa Shirika la Wafransiskani wa Maria Mkingiwa dhambi ya asili aliyetekwa nyara mwezi Februri mwaka huu huko Kusini mwa Mali Afrika, hali yake kiafya siyo nzuri.  Jenerali wa  kukundi cha ujenzi wa moja na uhuru wa mwanadamu (GAULA), ameyathibitisha hayo katika vyombo vya habari. Anasema, mtawa huyo  bado anaendelea kuishi japokuwa ana matatizo ya ugonjwa wa mguu na figo. Aidha Jenerali wa kikundi hicho amesema, yuko katika maandalizi ya utume mwingine kama mwakilishi wa  kikundi cha GAULA kwenda Afrika kukusanya haba zaidi ili kuweza kusaidia au kuchangia namna ya kumweka huru haraka iwezekanavyo kwa msada wa mashirika ya kimataifa.

Ikumbukwe wakati wa kutekwa nyara, padre Edmond Dembele Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu nchini Mali alikuwa ameliambia shirika la habari la Fides kuwa, wateka nyara walifika usiku wa tarehe 7 Febuari 2017 na pikiki ambapo waliacha mbali kidogo na kijiji alichokuwa anaishi Sisita Cecilia na watawa wenzake. Eneo hilo ambalo mpaka sasa linaendelea kukumbwa na vitendo vya ugaidi, linapatikana karibu na mpaka na Burkina Faso, zaidi ya kilomita 300 mashariki mwa mji wa Bamako. Kwa mujibu wa Wizara ya Usalama ya Mali, walikuwa wamethibitisha kuwa watu wanne wenye silaha walijitangaza kuwa ni wana jihadi.

Watu hao walifika katika majengo ya watawa kutoka jamii ya Shirika la  WaFranciscan, na kuvunja mlango wa nyumba yao, waliingia ndani ya majengo na kuondoka na vifaa vyote, ikiwa ni pamoja na kompyuta, alisema  Padre Edmond Dembele, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Mali. Waliomba kwanza pesa, kisha walichukua funguo za gari la wagonjwa. Waliondoka na gari hilo, wakiwa pamoja na mtawa huyo kutoka nchi ya Colombia. Kama kilomita tano baada ya kuondoka katika mji huo, watekaji nyara walitelekeza gari na kuliacha mahali walipokuwa wameacha   pikipiki walitoweka na mtawa lakini  wakaacha vifaa vya compyuta.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.