Padre Tersito Chito Soganub , katibu wa Mkuu wa Jimbo la Marawi aliyekuwa ametekwa nyara na kikundi cha magaidi wa Serikali ya kiislam nchi Ufilippini, ameachiwa huru kwa njia ya operesheni ya wanajeshi wa ufilippini kwenye usiku wa tarehe 16 Septemba 2017, kwa mujibu wa habari zilizoenea katika vyombo vya habari huko Manila.
Padre alitekwa nyara pamoja na kundi la waamini tarehe 23 Mei 2017 huko Marawi
Kusini mwa Ufilippini. Pade Chito amewekwa huru kwa njia ya operesheni kali ya wanajeshi
karibu na Msikiti wa Bato moja ya ngome kubwa ya kikundi cha magaidi cha Maute wanao
husika na utekaji nyara huo.
Taarifa zinasema, pamoja naye, alikombolewa hata na mateka mwingine ambapo mamlaka
wameweza kumtambua ni nani japokuwa hawakutaja jina lake. Hali ya vurugu huko Marawi
Ufilippini imekuwa ni uwanja wa michezo ya kivita kati ya jeshi na magaidi kwa miezi
hii ambapo imesababisha maelfu ya watu kukimbia pia uwepo wa uharibifu mkubwa wa maeneo
ya mji huo.
Na kwa njia operesheni kali ya mgogoro huo inaonesha kuwa mwisho kwa njia ya maaskari wanahusika katika shughuli ya kuwasaka magaidi. Pamoja na hayo viongozi wa Serikali wanasema ili kuweza kufanya ujenzi wa mji wa Marawi, utahitaji mabilioni ya mapesa ya Ufilippini. Naye Rais wa nchi ya Ufilippini Bwana Duterte amesema, mfuko wa fedha za kwanza uliokuwa umepangwa wa euro 820,000 hazitaweza kutosha katika ujenzi wa mji huo.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |