2017-09-16 11:24:00

Papa Francisko kutembelea Jimbo kuu la Bologna, tarehe 1 Oktoba 2017


Tarehe 1 Oktoba 2017 Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa kufanya ziara ya kitume Jimbo Kuu la Bologna. Ziara yake inatarajiwa kuanza asubuhi na mapema, lakini kwanza atasimama kitambo  Jimboni Cesena  mahali ambapo atafanya makutano na maadhimisho kidogo kwa mjibu wa taarifa za ratiba iliyotolewa. Askofu Mkuu Matteo Zuppi wa Jimbo Kuu la Bologna  anaeleza juu ya maandalizi ya kumpokea Baba Mtakatifu Francisko, ambaye anasema amewahi kusikia wanazungumzia juu ya Bologna, kwa njia hiyo anaamini kwamba atawafundisha mengi katika mikutano anayotarajiwa kufanya siku hiyo. Kadhali atawasadia hata wao  kukumbuka  kwa mara nyingine tena juu ya kutambua historia yao, uwezekano wao na urithi na tunu msingi za mji wao walizo nazo. 

Katika Altare itakayo tayarishwa kwa ajili ya madhimisho ya Misa  Kuu ya hitimisho la Kongamano la Ekaristi, itajengwa ikiwakilishwa na nguzo za mji kama ishara ya mapokezi ya watu wa Mkoa wa Emilia Romagna katika kielelezo cha maandishi ya Kardinali Gaicomo Lercaro Askofu Mkuu wa Bologna wakati wa kipindi cha Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican alisema "Ikiwa tunashiriki mkate wa mbinguni, tunawezaje tusishirikiane mazao ya nchi?". Askofu Mkuu Zuppi anaongeza kusema, na  hiyo ndiyo imekuwa  kauli mbiu ya Kongamao la Ekaristi Takatifu ambalo Baba Mtakatifu anakuja kuhitimisha  kwa upendo wa Kikristo katika Jimbo Kuu la Bologna.

Katika ratiba ya siku  ya Ziara ya Baba Mtakatifu Francisko Mjini Bologna, inajikita katika matukio ya aina sita,  ikiwa ni pamoja na makutano wa wahamiaji, kuzungukia barabara za kihistoria za mji   wa Boligna, Mahubiri na sala ya Malaika wa Bwana katika uwanja mkubwa, kukutana na watu maalumu na wafanyakazi.Aidha, Baba Mtakatifu atapata chakula cha mchana na maelfu ya maskini katika Madhabahu ya Mtakatifu Petronio na kukutana na  Mapadre na watawa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Ulimwengu wa kitaaluma kwa vijana wa vyuo vikuu watasikia neno lake katika uwanja wa Mtakatifu Domeniko, kabla ya Maadhimisho ya Misa Takatifu itakayofanyika katika Uwanja wa Mpira wa Ara mjini Bologna Italia. Mara baada ya Misa Takatifu, Biblia 100,000  zitatolewa kwa watu, kama ishara ya tukio la Jumapili ya kwanza ya Neno, kwa matashi ya Baba Mtakatifu mwenyewe ikiwa ni matunda ya Jubileo ya Huruma.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.