2017-09-07 14:37:00

Ask. Mkuu mstaafu Kard. C. Caffarra wa Jimbo Kuu Bologna Italia ameaga dunia


Kanisa Katoliki linaomboleza tena kwa Kifo cha Askofu Mkuu  Kardinali Carlo Caffarra, wa Jimbo Kuu La Bologna kilichotokea tarehe 6 Septemba 2017. Naye Askofu Mkuu Matteo Zuppi wa Jimbo Kuu  Bologna bchini Italia, anaelezea kwa uchungu mkubwa kwa niaba ya Jimbo lake  kuondokewa na Askofu Mkuu mstaaf. Anawaalika  mapadre  na waamini wote wenye mapenzi mema wa jimbo Kuu kuunganika naye katika maombi kwa ajili ya roho ya marehemu Kardinali Caffarra. Misa ya kumwombea itakuwa Ijumaa tarehe 8 Septemba 2017 saa tatu usiku katika Kanisa Kuu la Bologna. Aidha Askofu Mkuu Matteo Zuppi ataadhimisha misa ya mazishi, Jumamosi 9 Septemba saa tano sa asubuhi katika Kanisa Kuu Bologna na baadaye kufuata mchakato wa mazishi ndani Kanisa Kuu Bologna.

Katika maisha yake ya upendo na kuongozwa katika wito wake, Kardinali Carlo Caffara, Askofu Mkuu mstaafu wa Bologna, yamemwongoza  hadi kufikia siku yake ya mwisho kurudi kwake Mungu. Ushuhuda huo umekuwa mfano wa kuigwa na mapadre, familia na vijana katika kujifunza na kuhudumia Kanisa.  Marehemu Askofu Mstaafu Carlo Caffarra alikuwa na miaka 79 aliyoadhimisha tarehe moja Juni mwaka huu na kuliongoza  Kanisa la  Bologna kwa miaka karibu 12 na ameaga dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu. Alikuwa mtaalaam wa  mafunzo ya  familia na ndoa kwani ndiye aliye tumwa na Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili kuanzisha na kuendesha Chuo cha Kipapa cha Yohane Paulo II katika Mafunzo ya Ndoa na Familia.
Aliteuliwa kuwa Kardinali na Papa Mstaafu Benedikto XVI mwaka 2006 na alishiriki katika Mkutano Mkuu wa uchanguzi  wa Baba Mtakatifu Francisko 2013. Atakumbukwa sana kutokana kwamba, yeye pamoja na makardinali  wengine watatu yaani, Walter Brandmüller, Raymond L. Burke na Joachim Meisner ambaye tayari ni marehemu walisaini barua yao kuhusu  wasiwasi juu ya masuala kadhaa ya Waraka wa Papa wa Furaha ya Upendo wakiomba ufafanuzi zaidi.

“Siku chache baada ya kifo cha Kardinali Dionigi Tetamanzi, Kanisa letu la Italia linampoteza mwingine aliyetumikia Kanisa kwa moyo wote, akiwa rafiki na ndugu”. Ni maneno ya Kardinali Gualtiero Bassetti Askofu Mkuu wa Perugia na Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Italia mara bada ya kupata taarfa za uchungu wa kuondokewa na Askofu Mkuu mstaafu Carlo Caffarra.
Askofu Mkuu anasema akifirikia tu kwa urahisi mchango ambao ameutoa katika Baraza la kudumu, watajisikia wadeni wake. Yeye alikuwa ni mchangamfu, mwenye akili na amejiandaa vema kitaaluma. Alikuwa ni mwenye uwezo wa utambuzi ambao leo hii anaukabidhi kwake Bwana aliye mwamini na kumtumania katika  maisha yake yote.

Akieleza katika Gazei Katoliki la Avvenire, Askofu Mkuu Bassetti  anasema yeye binafsi alipata fursa ya kushirikishana naye katika mzunguko wa Sinodi ya maaskofu ya mwisho kuhusu familia.  Katika mchango wake katika hotuba alikuwa na msimamo mkuu na utambuzi wa misingi ya familia, wakati huo alitambua vema kuwa na karibu  hata kuwa na huruma  mbele ya  wale walio kuwa wakikosea iwe kwa upande wa marafiki au ndugu. Alitambua kuelezea kwa uhakika masuala makuu ya kibiadamu.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.