2017-09-06 15:01:00

Papa Francisko anasali kwa ajili ya wananchi wa Venezuela!


Baba Mtakatifu Francisko wakati wa hija yake ya kitume kuelekea nchini Colombia, Jumatano tarehe 6 Septemba 2017 amepata nafasi ya kuzungumza na waandishi wa habari ambao wako kwenye msafara wake, ili kuwasalimia na kuwatakia kazi njema. Baba Mtakatifu amewasihi waandishi wa habari wamsaidie katika utume huu nyeti na tete, ili Colombia ianze tena kutembea katika njia ya haki, amani na maridhiano. Baba Mtakatifu amewaomba waandishi wa habari kusali pia kwa ajili ya kufanikisha hija hii ya kitume. 

Ametanguliza shukrani zake za dhati kwa huduma makini wanayoitoa kwa ajili ya kuwajulisha watu, kile kinachoendelea katika hija yake ya kitume! Baba Mtakatifu kwa namna ya pekee kabisa, amewataka waandishi wa habari kusali kwa ajili ya kuombea Venezuela ambayo kwa sasa inakabiliwa na hali ngumu sana ya kisiasa, ili mchakato wa majadiliano uweze kuanza tena na amani ikite mizizi yake kati ya watu!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.