Kushuhudia huruma ya Mungu na kuondokana na ubinafsi wa kujitosheleza mwenyewe.
Ni moja ya maneno ya moja kwa moja katika lugaha ya Kihispania ya Baba Mtakatifu
Francisko alipokutana na Jumuiya chama Katoliki cha Kitume Shalom tarehe 4 Septemba
2017, ambapo wanachama wake wamepokelewa na kuongea na Baba Mtakatifu katika ukumbi
wa Mwenye heri Paulo wa VI mjini Vatican.
Mazungumzo wakati mwingine yaliyo kuwa yenye matani mengi, lakini yaliyo jaa utajiri
mkubwa na mawazo halisi ya maisha ya vijana wakati huo washiriki walikuwa ni 4000.
Kabla ya hotuba yake ya moja kwa moja na wazi, kwanza kulikuwapo na ushuhuda wa uzoefu
wa baadhi ya wanachama wa Shalom na ambayo Baba Mtakatifu aliwajibu kwa lugha rahisi
na wazi.
Baba Mtakatifu amesema, majibu aliyo yatoa ya jumuiya Katoliki ya Shalom iliyoanzishwa miaka 35 iliyopita, zaidi ni wito wa kushuhudi huruma. Ninyi hamwezi kuongea juu ya huruma badala yake ni kushuhudia, kushirikishana, kufundisha kuondokana na ubinafsi. Ni lazima kutangaza kwamba Mungu ni mwema ambaye anasubiri watu hata katika kipindi kigumu cha maisha.Papa anatoa mfano kuhusiana na hilo katika mfano wa mtoto mpotevu ambaye anasema kuwa baba yake alimsubiri, alipomwona kwa mbali alimwonesha nini maana ya huruma. Kutokana na hilo Papa amewaonya vijana ambao wanapenda kujitosheleza wao wenyewe, kuwa wabinafsi, kujifikiria wao weyewe na kwamba katika utamaduni tunamoishi, umejaa ubinafsi, ambapoanasema ni dozi ya kujipendelea, kujifikiria binafsi, kuwabeza wengine au kudharau wengine.
Hiyo ni hali ya kutoa huzuni kwasababau ni kuishi kwa mahangaiko ya kupamba na roho ya ubinafsi kila siku kwa sababu ya kutaka kuonekana bora au mwenyewe na kumbe siyo hivyo. Kwa njia hiyo usijitazame katika kioo ambacho kinadanganya, badala yake watazame wengine. Baba Mtakatifu amewapa ushauri kwamba kila siku wanapojiangalia katika kioo bora kujifunza kujicheka wenyewe, kwani katika utambuzi wa kucheka mwenyewe, inaweza kuleta furaha na kuona kishawishi cha kuwaambukiza hata wengine badala ya kujipendelea binafsi.
Halikadhalika Baba Mtakatifu amegusia pia suala la madawa ya kulevya , kutokana
na kijana aliyetoa ushuhuda wa kuondokana na janga hilo. Anasema, madawa ya kulevya
ni moja ya zana ambayo imo duniani tunamoishi na inazaidi kutawala na inazidi kutanda
mizizi katika familia za leo, zilizopita, hata katika upendo na katika yote.Kilio
cha Baba Mtakatifu ni kuona kwamba, kuishi katika dunia bila mizizi, hiyo ndiyo janga
la madawa ya kulevya naili kuweza kuondokana na madawa ya kulevya ni njia mojawapo
ya utambuzi wa hakika kwamba inawezekana kabisa kutengeneza mambo mapya na mema.
Katika kuelezea juu ya hili, amekumbusha juu ya safari ya Sinoni ya Vijana ambapo
amesema,wote ni lazima kuwa na mang’amuzi ya wito kwa ajili ya kutazana nini Bwana
anataka katika safari ya utume, yaani kujitoa bila kubakiza kile ambacho tumepokea
bure. Huo ndiyo wito wa nguvu ambao ameutoa kwasababu anasema kutoa bure ni kujaza
roho.
Tafakari la mwisho lilikuwa linahusu mtu mwenye umri mkubwa kwa maana ya uzee katika
Jumuiya ya Shalom , amewasisitizia juu ya mazungumzo kati yao na vijana, kwamba ndiyo
moja ya changamoto za ulomwengu huu. Vijana kwa thati wanahitaji kusikiliza wazee,
kama pia ilivyo kwa wazee kuwasikiliza vijana. Onyo lake Baba Mtakatifu anasema,
wazee hawapaswi kuwekwa kabatini kama nguo zilizokunjwa na kuhifadhiwa ndani yake.
Ametoa mfano huo, kutokana na uzoefu wake alio ufanya hapo zamani kwamba, alikwenda
na kikundi cha vijana katika nyumba ya wazee, vijana hao walipiga vyombo vya muziki
na kutumbuiza, baada ye walianza mazungumzo, ambayo yalikuwa kati ya bibi na wazee
ambayo yalikuwa ya hekima.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |