2017-09-04 10:06:00

Papa:Amekumbuka waathirika wa mafuriko barani Asia na ziara ya Colombia


Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana Baba Mtakatifu amewakumbuka watu waliopata maafa ya asili na kuwatia moyo na karibu katika kushiriki mateso ya watu hao katika mafuriko Barani Asia ya mashariki,pia kimbunga cha kutisha huko Texas na Louisiana. Amesema wakati akiwa anarudia kwa upya kuwa karibu kiroho kwa watu wa Asia ya mashariki wanaoendelea kuteseka kutokana na maafa ya mafuriko, anapendelea pia kuwa karibu na mateso ya wakazi wa Texas na Lousiana ,waliopata janga la kimbunga na kusababisha mvua za kutisha, mahali ambapo yamesababisha waathirika wengi na maelfu ya watu kukosa makazi na kupoteza mali zao zote. Kwa maombezi ya Mama Maria Mtakatifu tulizo la wenye taabu awaombee kwa Bwana wapate neema ya kuvumilia ndugu hawa walio jaribiwa.

Aidha amewashukuru kikundi cha watu waliokuwa katika kiwanja na matangazo ya kumtakia safari njema , Baba Mtakatifu pia amegusia juu ya ziara yake ya kitume itakayo anza tarehe 6 Septemba na kurudi Vatican tarehe 11 Septemba, amewashukuru wote waliomtakia mema katika safari hiyo.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.