2017-09-02 08:48:00

Ujumbe wa Papa kwa njia ya Video:Tuombee Parokia zetu zifungue milango wazi


Kila mwezi Baba Mtakatifu Francisko anatoa ujumbe kwa nia ya mwezi kwa njia ya Video ambapo katika  mwezi  wa  tisa mwaka huu nia zake  zimelenga kuhusu  parokia ambapo nasema;" parokia zote zinapaswa kuwasiliana na familia na kushiriki kikamilifu katika maisha ya watu"
Baba Mtakatifu anasisitiza, "Parokia zinapaswa kuwa nyumba zenye milango iliyo wazi ili kuweza kukutana na wengine. Ni muhimu kwenda kukutana na wengine ili kukuza imani; na hiyo inawezakana  tu kutokana na kuacha milango wazi ili Yesu aweze kutoa ujumbe wake wa furaha".
Anamalizia kwa kusema Baba Mtakatifu, "tuombee Parokia zetu ili kwamba zisigeuke kuwa ofisi za wafanyakazi wa mishahara bali ziongozwe na roho ya kitume na kuwa sehemu ya kukuza imani na ushuhuda wa upendo".

Huu ni ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko kwa njia ya video kila mwezi ulio anzishwa na Mtando wa Kimataifa kwa ajili ya Maombi ya Papa kwa ushirikiano wa Kituo cha Televisheni cha Vatican. Katika Video zinonekana picha za vijana wakitoka katika parokia moja kwa jitihada za kutoa mshikamano na msaada kwa wale wahitaji zaidi.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 
All the contents on this site are copyrighted ©.