2017-09-02 16:33:00

Papa:Ulimwengu wa leo unahitaji ushuhuda wa ushirikiano kati yetu


Jumamosi tarehe 2 Septemba 2017, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na kutoa  hotuba yake kwa washiriki wa Mkutano wa Baraza laViongozi wa kidini nchini Korea akiwakaribisha kwa furaha kubwa.  Ameelezea jinsi gani wamefanya  safari ndefu kufika Roma kwa ajili ya kukamilisha hija yao ya kidini. Amewashukuru na kwa namna ya pekee Askofu  Mkuu  Hyginus Kim Hee-jong, wa Jimbo Kuu la Gwangju na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Korea aliyefikiria kufanya tukio hilo pia kwa maneno ya hotuba yake. Baba Mtakatifu anawakumbusha maneno aliyo nena wakati wa ziara yake huko Seoul 2014 kwamba, maisha ni safari ndefu lakini ambayo siyo rahisi kusafiri pekee. Ni lazima kusafiri na ndugu mbele ya uwepo wa Mungu. Hivyo anasema  leo hii wametimiza hatua nyingine ya kutembea pamoja.

Kama mjuavyo hawali ya yote tangu  Mtaguso wa II wa Vatican na kuendelea, Kanisa Katoliki halichoki kamwe kutembea katika njia ambazo wakati mwingine siyo rahsi, za majadiliano na kuhamasisha kwa namna ya pekee kuwa na mazungumzo na madhehebu mengine. Hata leo hii Kanisa linatoa wito kwa waamini wake ili kwa umakini na upendo watambue, kutunza na kuendeleza thamani za kiroho, kimaadili na utamaduni ambazo zinapatikana kwa kila mmoja (Nostra Etate, 2). Mazungumzo ya kidini yanayo fanyika kwa njia ya kuwasiliana, mikutano na ushirikiano ni mapana na yenye thamani ambayo ni utashi wa mwenyezi Mungu pia ni changamoto kwa ajili ya wema wa pamoja na amani.

Baba Mtakatifu Francisko anasisitiza kuwa, mazungumzo yanayohitajika ni lazima yawe wazi kwa kulinda  heshima na kwa njia hiyo yanaweza kuzaa matunda. Kuwa wazi maana yake ni kukubaliana, kuwa wa kweli ambapo mtu anakubali kutembea pamoja na kumsifu Mungukwa dhati. Kuheshimu maana yake ni kuheshimiana mmoja na mwingine ambayo ni wajibu na sheria; na  wakati huo huo ni maisha na mazungumzo ya kidini. Pamoja na hayo ni katika kuheshimu haki ya maisha, ya kushirikishana kimwili hadi uhuru msingi kama ilivyo hata dhamiri, dini, fikra, kujieleza, ambavyo ni vitu msingi mkuu wa amani na ambavyo  kila mmoja anaalikwa kuomba na kuwajibika katika utekelezaji.

Ulimwengu unatazama sisi na unataka kushirikiana kati yetu na watu wote, waume kwa wake wenye mapenzi mema. Baba Mtakatifu Francisko anafafanua nini maana yake kwamba, ulimwengu unahitaji jibu na kuwajibika katika kushirikishana mada mbalimbali zinazoikumba dunia kama vile utakatifu wa hadhi ya mtu, njaa na umasikini ambao ni mgogoro mkubwa kwa watu walio wengi, kupinga migogoro kwa namna ya pekee kwa wale wanao tumia jina la Mungu kunajisi maisha ya binadamu na mambo ya kidini, ufisadi unaozidi kuongezeka na kusababisha ukosefu wa haki msingi, kumomonyoka kwa maadili, kipeo cha familia, uchumi, mazingira, na siyo mwisho bali hata matumaini.

Kwa njia hiyo bado kuna safari kubwa ya kitimiza pamoja kwa unyenyekevu, bila kuchoka,na hata bila kupaza sauti juu, bali kujikita kwa kina zaidi katika kupanda mbegu ya matumaini ili kuweza kuwasaidia binadamu wengi. Ni  kuweza kusikiliza vilio vya wengi ambao wako katika mgogoro wa vita wakiomba kusikilizwa kati ya watu, jumuiya, watu wote na mataifa. Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu anasisitiza kuwa, viongozi wa kidini wanaalikwa kufungua, kuhamasisha na kusindikiza mchakato kwa ajili ya wema wa mapatano ya wote. Aidha wote tunaalikwa kuwa watafutaji kwa hali zote  amani, kutangaza na kujivisha ile njia ya kutokutumia nguvu. Aina ya amani kwa kujiamini pia kujieleza bila kuwa na woga, aidha kwa ishara ambao zinapinga aina yoyote ya chuki.

Amehitimisha hotuba yake Baba Mtakatifu, katika mkutano huo unathibitisha safari yao. Kuwatazama pale kama mahujaji imemkubusha juu ya hija yake nchini Karea ambapo bado anaendelea kumshukuru Mungu na watu wake wapendwa, ambao yeye mwenyewe hachoki kila siku kuomba Mungu zawadi ya amani na mapatano ya kidungu. Anakumbuka urafiki na mema mengi aliyoyapokea  na kwamba yanasaidia kuendelea na safari hiyo pamoja kwa msaada wa Mungu.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.