2017-08-31 18:32:00

Card.Turkson amehutubia juu ya amani na Ulinzi wa Viumbe huko Astana


Katika Onesho la Kimataifa la EXPO 2017 ambalo limefunguliwa huko Astana nchini  Kazakhstan linaloongozwa na kauli mbiu “Nishati ya baadaye” pia katika onesho hilo hata Vatican ni mshirik wa maonesho yake katika banda lake lenye kauli mbiu “Nishati kwa ajili ya wote: kutunza nyumba yetu ya pamoja”. Katika fursa hiyo naye Kardinali Peter Turkson Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Endelevu ya Binadamu yupo mjini humo  tangu tarehe 30 Agosti hadi tarehe 4 Septemba 2017 kushiriki katika tukio hilo. Tarehe 31 Agosti amefanya mkutano  na viongozi wa madhehebu ya dini kuhusu amani na ulinzi wa viumbe,  mkutano ulio andaliwa na Baraza lake.

Katika hotuba yake Kardinali Turkson amewasalimia washiriki wote wa dini na wa kisiasa walio kuwapo,na  kuweka bayana matatizo yanayoikabili sayari hii kutokana na matumizi mabaya binafsi na pia   kutokuwapo mfumo bora  wa mgawanyiko sawa wa rasilimali za ardhi hii, ameitaja kuwa mojawapo ni nishati. Kwa njia hiyo ametaja changamoto kubwa   inayoikabili  sayari hasa   hali ya kuongezeka kwa joto dunia,  ukame, kukatwa misitu hovyo, mmomomyoko wa udongo, kuyeyuka kwa barafu, maafa ya asili kama vile mafuriko, vimbunga, tetemeko la ardhi, kupungua kwa baadhi ya wanyama na mambo mengine yanayo husu Sayari hii.

Kardinali Turkson  amechambua  kwa kina matukio mengi yanayowakumba mamilioni ya watu  na zaidi kuonesha nchi nyingi zinazoendelea. Amesema kama viongozi wa madhehebu ya dini ni dhahiri kwamba siyo rahisi kupata ufumbuzi sahihi, lakini pia inawezakana kuwa na mtazamo wa upeo wa juu wa dunia na hasa unaoongozwa na imani. Kila mwamini katika Sayari hii lazima atazame kwa upya namna ya kuishi. Lazima kutafuta kila njia na kutoa shukrani kwa Mungu kwa zawadi zake kama hewa, upepo, maji , ardhi moto, na chakula. Amesisitiza kwamba, ni kurudia kwa upya  namna ya kutumia ardhi yetu kwa  utaratibu katika matumizi sahihi ya rasilimali za ardhi hiyo.

Ni lazima  kuongozwa na kanuni ya upeo na msingi ya kwamba dunia inaelekea wapi na mali zake za asili kama ardhi ili kuweza kuwashirikisha wengine katika familia ya wanadamu wote na kuwa na hisia ya kuwajibika. Hiyo yote anasema, ni kwasababu ya kuweza kuzuia majanga ya asili na kuwa na huduma halisi ya uumbaji.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.