2017-08-22 10:12:00

Papa: Ujumbe wa Siku ya Wahamiaji na Wakimbizi Duniani kwa Mwaka 2018


Papa Francisko anasema, "Wakati wa kuanza utume kama Papa , nimerudia mara kwa mara kwa namna ya pekee juu ya wasiwasi kutokana na uchungu wa wahamiaji wengi wanaokimbia vita, mateso, majanga ya asili na umaskini. Hizi ni hali za ishara za nyakati, ambazo nimejaribu kutafakari matukio haya nikiomba mwanga wa Roho Mtakatifu tangu nilipotembelea Lampedusa tarehe 8 Julai 2013. Katika kufanya mabadiliko ya Baraza jipya kwa ajili ya Huduma ya Maendeleo endelevu ya binadamu, nilipendelea kwamba sehemu hii ya kijamii iwe chini ya Uongozi wangu , ili kuweza  kuhamasisha zaidi Kanisa juu ya wahamiaji , msongamano, wakimbizi na waathirika wa biashara ya binadamu ya binadamu".

Huu ni utangulizi wa Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko wa Siku ya Wahamiaji Duniani kwa Mwaka 2018 ulitolewa Jumatatu 21 Agosti 2017. Baba Mtakatifu Francisko anaandika; kila mgeni anaye bisha hodi katika milango yetu, ni fursa ya kukutana na Yesu Kristo, ambaye anajifananisha na mgeni wa  kukaribishwa au kukataliwa kila nyakati (Mt 25,35.43).Bwana anawakabidhi upendo wa umama wa Kanisa kila binadamu yoyote anayelazimika kuacha nchi yake akitafuta maisha bora ya baadaye. Wito huo unapaswa kujieleza kwa dhati kila hatua ya uzoefu wa wahamiaji kwa maana ya kuanzia safari  hadi kufika na kurudi tena. Ni uwajibu mkubwa ambao Kanisa linataka kushirikisha wote, kwa waamini , wake kwa waume wenye mapenzi mema ambao wameitwa kujibu kwa upendo, hekima, mtazamo mwema , na kila mmoja kadiri ya uwezo wa kila mmoja.

Kwa upande wa suala hili, Baba Mtakatifu anasisitiza kwa kuyaweka katika vipengele vya maneno manne ya mafundisho ya Kanisa yaani kukaribisha , kulinda, kuhamasisha na kushirikisha. Amefafanua kila kipengele akisema; katika kufikiria matukio ya sasa, kukaribisha maana yake  hawali ya yote ni kuwezesha wahamiaji na wakimbizi uwezekano mpana wa kuingia kwa usalama na halali katika nchi wanazotamia. Kwa maana hiyo inatakiwa shughuli madhubuti ya kuongeza juhudi katika kuharakisisha ruhusa ya visa ya binadamu ili waweze kuwafikia familia zao. Hata hivyo, Baba Mtakatifu anawaomba kwamba idadi kubwa ya nchi waweze kukubali mipango ya  wafadhili(Sponsorship) binafsi na jummuiya za kuweza kufungua mikondo ya kibinadamu kwa ajili ya wakimbizi zaidi walio athirika.Vilevile ingekuwa ni mwafaka kutoa visa ya muda mfupi na hasa kwa watu ambao wanakimbia migogoro katika nchi jirani.

Kuhusiana na suala la kuwarudisha wakimbizi, Baba Mtakatifu anasema siyo suluhisho la kuwarudisha kimkumbo wahamiaji na wakimbizi hasa wale wanaotoka katika nchi ambazo haziweze kuhakikisha heshima na adhi msingi ya binadamu. Kwa njia hiyo anasisitiza umuhimu wa kuwasadia na kuwawezesha wahamiaji na wakimbizi maeneo yanayoridhisha. Mipango ya mapokezi iliyotawanyika  katika maeneo tayari mengi anafikiri kwamba inasaidia kwa kiasi fulani  makutano binafsi ili kuwawezesha kuwa na hudumazilizo bora na zenye kufaa. Aidha anasisitiza kuwa kiini cha msingi wa Binadamu,kama ilivyoelezwa na Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto wa XVI inatoa ulazima wa  kuweka usalama binafsi na ule wa taifa. Kwa njia hiyo ni lazima kuwapo wataalamu wa uchunguzi katika mipaka.

Hiyo ni kwasababu hali ya wahamiaji wanaotafuta hifadhi na wakimbizi, wanahitaji uhakika wa usalama wao binafsi na hupatikanaji wa huduma msingi,kwa njia hiyo, kwa jina la heshima msingi ya kila mtu ni lazima kujitahidi kutafuta njia mbadala kwa wale wanaoingia katika nchi bila ruhusa.
Kipengele cha pili ni kuhusu  kulinda, ni kitendo linachojikita katika aina mbalimbali za matendo ya ulinzi wa haki na hadhi ya wahamiaji na wakimbizi, bila kujali hali yao ya kuhamahama. Ulinzi huo huanzia nyumbani kwao, na hasa zaidi uanzie katika utoaji wa taarifa fulani na kuthibitishwa kabla ya kuondoka kwao, hiyo ni kwasababu ya ulinzi wao ili kuodokana na ukiukwaji wa sheria ya kuingia bila vibali.Hiyo ingeweza kuendelea kwa kiasi fulani iwezekanavyo katika nchi ya uhamiaji kwa  kuhakikishia wahamiaji wanapata misaada ya kutosha na kitulizo, haki ya kutunza nyaraka zao na vitambulisho vyao binafsi,hupatikanaji wa haki sawa, uwezekano wa kufungua akaunti ya benki na dhamana ya kiwango cha chini cha maisha. Iwapo vitambulisho vyao vina fursa ya kutambuliwa thamani yake, uwezo na ujuzi wa wahamiaji wanaoomba hifadhi  na wakimbizi hawa wanawakilisha rasilimali kwa jumuiya ambazo zimewapokea.

Kwa njia hyo Baba Mtakatifu Francisko anaendelea kusema kuwa anayo  matumaini ya kwamba kwa heshima na utu wao, wanaweza kupata uhuru wa kwenda katika nchi zinazowapokea, uwezekano wa kufanya kazi na uwezekano wa mawasiliano ya simu. Kwa wale ambao wanaamua kurudi nyumani kwao, Baba Mtakatifu anasisitiza, wapate fursa ya nafasi ya kuendeleza mipango ya kitaalamu na kijamii,aidha kuwaunganisha na jamii. Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Mtoto hutoa msingi  wa kisheria kwa ajili ya ulinzi wa watoto  wahamiaji. Kwa ajili yao ni muhimu kuepuka aina yoyote ya kizuizi kutokana na hali ya kuwa wahamiaji, wakati huo ni lazima kuhakikisha  upatikanaji wa shule za msingi na sekondari. Kadhalika ni muhimu kuhakikisha mafunzo ya kudumu nyakati zijazo kulingana na umri wao  na uwezekano wa kuendelea na masomo yao. Kwa watoto wanaofika bila kusindikizwa au wametengana na familia zao ni muhimu kuunda mipango ya muda mfupi au kuwakabidhi katika malezi.

Kuhusiana na utaifa wa watoto, Baba Mtakatifu Francisko anaendelea; kwa sababu  ya haki kwa wote kwa taifa, wanapaswa kutambuliwa ipasavyo kuthibitishwa na kuandikishwa kwa watoto wote wavulana na wasichana wakati wa kuzaliwa, ili kuweza kepupka kukosa utaifa ambao wakati mwingine wanajikuta wahamiaji na wakimbizi. Inawezekana ki urahisi kuzuiwa kwa njia ya kuandikishwa uraia kwa mujibu wa kanuni za sheria za kimataifa. Hali za wote wanaohama isiwe kizuizi cha upatikanaji wa huduma ya afya na pensheni ya kitaifa, ikiwa ni pamoja na uhamisho wa michango yao ikitokea kurudishwa makwao.

Kuhamasisha maana yake ni uwezo msingi wa kuhakikisha kwamba wahamiaji wote na wakimbzi kama pia jumuiya ambazo zinawapokea, waweze kuwekwa katika hali inayorodhisha katika kipimo cha ubinadamu aliyependwa na Muumba. Kati ya vipimo hivyo , ni lazima kutoa thamani ya haki na mwelekeo wa kidini, kuhakikisha kwamba wageni wote waliopo katika eneo wanao uhuru wa kukiri imani yao. Wakimbizi na wahamiaji wengi wana ujuzi ambao unapaswa kuthibitishwa na kutolewa  thamani yake. Kwa kuwa "kazi ya binadamu, kwa tabia yake ina maana ya kuunganisha watu," Baba Mtakatifu Francisko anawatia moyo wa kufanya kila linalowezekana ili waweze  kuhamasisha na kukuza ile hali ya kuwaunganisha kijamii katika kazi wahamiaji na wakimbizi, kuhakikisha ni kwa wote ikiwa ni pamoja na wanaotafuta hifadhi uwezo wa kufanya kazi, mafunzo lugha na kazi ya uraia ya kutosha katika  lugha zao za asili.

Kwa upande wa watoto wahamiaji, inahitajika kazi ya kushirikiana kwa pamoja  kwa namna ya kuweza  kuzuia matumizi mabaya na vitisho na hathari dhidi ya ukuaji wao wa kawaida. Mwaka 2006, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI alionyesha jinsi gani suala ya familia za wahamiaji kuwa ni rasilimali ya utamaduni wa maisha na sababu ya kuunganisha thamani na maadili.Uadilifu wake lazima ukuzwa, kwa kutafuta jinsi ya kuwaunganisha pamoja na familia zao na ndugu zao kama babu na bibi, na ndugu wengine bila kutegemea tu mahitaji ya kiuchumi. Kwa upande wa hali ya wahamiaji na wakimbizi wanaotaka hifadhi katika hali ya ulemavu, lazima kuwalinda na kuwahakikishia zaidi  umakini na msaada.Wakati kuzingatia juhudi kubwa  hadi sasa za nchi nyingi katika suala la ushirikiano wa kimataifa na misaada ya kibinadamu, Baba mtakatifu Francisko anayo matumaini ya kwamba katika ugawaji wa misaada hiyo itakuwa ni kuzingatia mahitaji (kwa mfano, huduma ya afya, jamii na elimu) ya nchi zinazoendelea  ambazo zinapokea mtiririko mkubwa wa wakimbizi na wahamiaji, vivyo hivyo,wanajikuta katika hali mbaya  hata wale waliopokea kwa ukosefu wa zana na kuishi katika mazingira magumu.

Neno la mwisho, ni kushirikisha, Baba Mtakatifu Francisko anaeleza juu ya neno hili kuwa, hii inahusiana na fursa ya nafasi ambayo ni utajiri wa utamaduni unaotokana na uwepo wa wahamiaji na wakimbizi.Kushirikishana hauna maana ya kufananishaambao utaka kukandamiza au kusahau utamaduni wao wenyewe au utambulisho. Kumbe kuwasiliana na wengine husababisha kugundua siri ya kuwa wazi na kukaribishana na kupekeana katika masuala mbalimbali na kuchangia uelewa mkubwa wa pamoja. Ni mchakato wa muda mrefu na hivyo una lengo la kuunda sura ya jamii na utamaduni kuwa zawadi ya Mungu kwa watu.Mchakato huu unaweza kuwa wa kasi kwa njia ya kutoa  ofa ya uraia usiyo ingiliana na  mahitaji ya kiuchumi kama vile  lugha na mipango ya mafunzo halali kwa namna ya pekee kwa wahamiaji ambao wanaweza kukaa kwa muda mrefu katika nchi. Kwa namna hiyo Baba Mtakatifu anasisitiza tena muhimu wa kukuza kwa kila njia utamaduni wa kukutana na kuzidisha fursa kwa ajili ya kubadilishana utamaduni, kuhifadhi na kusambaza mbinu bora za ushirikiano na kuendelezamazungumzo na kujiandaa kijamii katika mchakato kamili.

Kwa mujibu wa mila na desturi za uchungaji, Kanisa liko tayari kujikita katika kutekeleza mipango hawali ya yote ya binadamu iliyopendekezwa, lakini ili kuweza kupata matokeo yanayotarajiwa ni muhimu kwamba jamii nzima ya kisaisa na raia wote pamoja kila mmoja kulingana na majukumu yake kujikita barabara katika utekelezaji wa maelekezo hayo. Baba Mtakatifu pia anaeleza; wakati wa Mkutano wa Umoja wa Mataifa, mjini New York tarehe 19 Septemba, 2016, viongozi wa dunia walionyesha wazi  nia yao ya kufanya juhudi kwa ajili ya wahamiaji na wakimbizi na  kuokoa maisha yao na kulinda haki zao, kwa kushirikiana  wajibu kwa ngazi ya  taifa. Hadi sasa nchi wanachama bado wanayo lengo na maandalizi ya kuidhinisha ifikapo mwishoni wa 2018 mikataba miwili ya kimataifa (Global Compacts), moja unahusu wakimbizi na mwingine ni wahamiaji.

Anamalizia akisema, katika mwanga wa taratibu wa michakato hii, miezi michache ijayo itawasilisha  fursa nzuri ya kusaidia hatua madhubuti ambayo Baba Mtakatifu amependelea kuitafsiri katika vipengele vinne. Anawaalika kuchukua fursa hiyo kwa kila mtu katika  nafasi kushirikisha ujumbe kwa  wote, kwa wahusika  wa kisiasa na kijamii au wadau katika machakato ambao utafikia kutoa idhini ya mikataba miwili ya kimataifa. 

Leo ni tarehe 15 Agosti wakati Kanisa linaadhimisha Sikukuu ya Bikira Maria kupalizwa mbinguni. Mama wa Mungu alifanya uzoefu mgumu wa uhamisho(Mt 2,15-15) alimsindikiza mwanae kwa upendo na hata katika njia ya msalaba,na sasa anshiriki utukufu milele. Kwa maombezi yake ya kimama, tunamkabidhi matumaini ya wahamiaji na wakimbzi wote dunaiani na matarajio ya jamii ambayo inawapokea, ili kwamba kwa mujibu wa amri kuu ya Mungu ,tunaweza wote kujifunza kupenda mgeni kama sisi wenyewe tunavyojipenda.
Vatican, 15 Agosti 2017
Sikukuu ya Bikira Maria Mpalizwa.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.