2017-08-17 09:49:00

Sikukuu ya Kupalizwa mbinguni Mama Maria kuadhimishwa na imani


Pamoja na matatizo makubwa yaliyoko katika nchi ya Siria, Jumuiya ya Kikristo imeungana kwa pamoja kuadhimisha sikukuu ya Kupalizwa Bikira Maria Mbinguni. Ni mwaka wa 7 sasa sikukuu hii kuangukia bado katika hali mbaya ya vita ambavyo vimeharibu nchi. Pamoja na hayo yote, wakristo wali bado wanaonesha matumani makubwa. Na Taarifa zaidi zinaonesha  bado mapigano yanaendelea katika Wilaya za Raqqa, Homs e Deir al Zur, katikakati ya nchi ya Siria ambayo imethibitiwa na serikali ya Kiislamu.

Mwandishi wa habari wa Radio Vatican ametaka  kujua zaidi roho ya wakristo wa huko Siria wakati wa kuadhimisha sikukuu ya Kupalizwa mbinguni mama Maria. Habari zaidi ni kutoka   kwa Balozi wa Kitume huko Damasko, Kardinali Mario Zenari ambaye amesema kuwa, sikukuu ya kupalizwa mbinguni katika Makanisa ya Mashariki ikiwa wengi ni wakatoliki wa kiorthodox wanaitambua kama sikukuu ya  kulala usingizi wa  mama Maria pia ikiwa  ni sawasawa na kanuni ya Kanisa (Dogma). Pamoja na hayo lakini  kuna jambo la kusisitiza katika makanisa ya mashariki na kilatini ya kwamba wana adhimisha siku hiyo hiyo ya tarehe 15 Agosti. Kardinali Zenari anasema waamini wameudhuria Kanisani kwa wingi wakiwa wanaimba nyimbo za Maria, lakini  wakati huo wakiwa wameanza na mfungo kabla ya sikukuu.

Alikadhalika ameelezea juu ya Sikukuu  ya mama Maria  inavyoheshimiwa hata kwa upande wa waislamu na kwamba katika nchi ya Siria daima kumekuwa na uhuru wa dini na wa kuheshimiana mmoja na mwingine, pia mama Mama Maria amekuwa akiheshimiwa sana, hata katika kurasa za Korani zinatambua Mama Maria kuwa ni mama wa Nabii, kwa maana hiyo nao wanashiriki katika hali ya sikukuu na wakristo. Mwaka huu ukiwa ni mwaka wa saba tangu kuanza kwa vita lakini kwa namana ya pekee watu wameanza kuonja hali ya utulivu, hata kama sehemu nyingine bado kuna mateso mengi.
Kardinali Zenari amesema ni katika maeneo ya Ragga ambayo watu wengi ilibidi wakimbie , inasemekana tangu Aprili mwaka huu wamefikia watu 200 elfu.

Baada ya miaka saba ya vita katika kipindi hiki kati ya Jumuiya za kikristo zinaweza kuishi na matumaini kwa siku zijazo kwa maana ya kwamba katika parokia tatu za eneo la Idlib amesikia kuwa  waamni 700 pamoja na vizingiti walivyo navyo wanao uwezo wa kuudhuria liturjia na sala kila siku kwa sasa. Balozi amesema  ni furaha gani ya jumuiya hizo pamoja na vizingiti lakini wameweza kufanya sikukuu ya Kupalizwa mbinguni mama Maria. Katika maeneo hayo mapokeo na utamaduni wa  Mama Maria ni wenye nguvu, na katika makanisa na nyumba nyingi za watwa zimeweka mama Maria kuwa msimamizi mahali ambapo watu wengi wanakwenda kusali kwa matumaini wakiomba  amani na  mapatano ya nchi ya Siria.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.