2017-08-17 10:46:00

Maaskofu wa India kuwatakia baraka raia wao ya miaka 70 ya uhuru


Miaka sabini iliyopita, nchi ya Pakistani na India  tarehe 14 na 15 Agosti 1947 walitangaza uhuru wao kutoka mikononi mwa Ukoloni wa Kingreza. Lakini matukio ya kihistoria  na kisiasa yalizidi kuendelea na mzozo kati ya nchi hizi mbili, matatizo hayo kwanza kabisa yalisababishwa na mvutano wa kanda ya Kashmir. Ki ukweli hali hiyo ya Pakistan na India leo hii iko  mbali na Muungano wa taifa kubwa ambao  Mahatma Ghandhi angependelea. Kwa mujibu wa Marzia Casolari, profesa wa historia ya nchi za Asia katika Chuo Kikuu cha Turin nchini Italia amesema, sehemu kubwa ya msuguano kati ya India na Pakstan itaweza kutatuliwa iwapo utafanyika mgawanyiko wa sehemu mbili kitaalamu wa Mkoa wa Kashmir wenye kuwa na mgogoro.

Katika maadhimiso  ya miaka 70 ya uhuru wa nchi hiyo; hata Kanisa Katoliki limeungana kwa pomoja katika maadhimisho hayo. Askofu Theodore Mascarenhas, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki  nchini India ametoa maoni yake akisema; wanashukuru Mungu kwa nchi hiyo kubwa yenye kuwa na ustaarabu mkuu,  kwa ukarimu wao uliyo waweza kupokea ukatoliki kwa miaka mingi. Askofu anasema, wanafurahi kuwa raia wa India na kuwa na ustaarabu ambao siku zote umekuwa utamaduni wa kuvumiliana na ushirikiano wa amani kati ya dini na jumuiya mbalimbali.
Wakiwa wanaadhimisha miaka  70 ya uhuru anaongeza, wanatarajia maendeleo endelevu katika nchi yao kubwa, hasa nchi ambayo inaweza kutoa kipaumbele kwa maskini, watu wa kiasili , wadalit na wale waliotengwa.Kwa maana watu hawa  wanabaki bado moyo wa Kanisa , kama Yesu mwenyewe alivyo fundisha.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.