2017-08-17 09:25:00

Maaskofu nchini Brazil kuandaa Mkutano wa 10 juu ya Mawasiliano


Tarehe16 hadi 20 Agosti ,katika Jimbo la Joinville, nchini Brazil umefunguliwa Mkutano muhuimu wa mawasiliano, ambao unafanyika kila baada ya miaka miwili unao andaliwa  na Baraza la Maaskofu  nchini Brazil. Mada iliyochaguliwa kuongoza mkutano wa waandishi wa habari na wahudumu wa mawasiliano ni kuelimisha  juu ya mawasiliano.Aliyefungua Mkutano huo kwa hotuba ni Monsinyo Dario Vigano, Rais wa Sekretarieti ya Mawasiliano (Spc) Vatican. Akiongea na Gazeti la Sir Monsinyo Vigano amesema ni mara yake ya pili kukaribishwa katika ufunguzi wa Mkutano huo wa Kanisa la Brazil ambao wameandaa mkutano wa mawasiliano katika mwanga wa mabadiliko ya kiteknolojia na hata kudhoofika kwa fursa mbalimbali za maisha ya watu.

Mwaka 2011 Kauli mbiu ya Mkutano uliofanyika  Rio de Janeiro ulikuwa ni “Mawasiliano na Maisha:katika utofauti na mzunguko wa maisha”. Kwa njia hiyo Monsinyo Vigano anasema mwaka huu kuna mabadiliko ya mada ambayo kwa namana ya pekee ni kujikita zaidi katika kuelimisha juu ya mawasiliano mema. Mafunzo kwa wanahabari na wahudumu wa mawasiliano ni mada muhimu sana ambayo Baba Mtakatifu Francisko amesisitiza sana wakati wa kuadhimisha Siku ya 51 ya Mawasiliano Duniani mwaka huu. Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake anasema, ni muhimu, ni mikakati ya kuwa na wahusika wakuu wa mawasiliano walio jiandaa vema, wanye uwezo wa kujua ni jinsi gani ya kuwa na uzoefu na utaalamu wa vyombo vya habari duniani kwa kufuata roho ya Injili.Aidha wakiwa na uwezo wa kupendekeza hoja  kwa wahusika wake waume na wake simulizi katika mantiki ya habari njema.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.