2017-08-17 14:39:00

Hotuba ya Mkutano wa Mwaka ya Umoja wa Ulaya kusubiriwa kwa hamu


Inasubiriwa kwa hamu sana hotuba kuhusu nchi wanachama wa Ulaya tarehe 3 Septemba 2017 ambayo Rais wa Tume ya Ulaya Jean-Claude Juncker atatamka mbele ya Bunge la Ulaya huko Strasburgo. Kila mwaka mwezi Septemba, Rais wa Tume ya Ulaya wakiwa katika meza ya mduara kwenye mkutano wa mwaka uwakilisha taarifa kamili ya mwaka.Hotuba ya Umoja wa nchi ya za Ulaya hutoa msimamo wa hali halisi ya mwaka mzima ambao unakuwa umemalizika, pia kuonesha mikakati mipya ambayo ni ya kupewa kipaumbele kwa nyakati zijazo. 

Halikadhalika Mkutano huo wa mwaka unatoa mazungumzo na maagizo ya programu kwa ajili ya utaratibu wa utendaji kwa kila mmoja wa nchi mwanachama. Kwa kipindi hiki, Rais anaweka bayana akiwa katika Ukumbi wa Berlaymont kwa kuonesha jinsi gani Tume inatarajia kujibu changamoto zinazoikabili Bara na jinsi ya kuweza kupambana nayo.Hata hivyo taarifa inaonesha kuwa katika hotuba  ambayo Junker anaiandaa akiwa na timu yake na Kamishna wa Baraza, wanafanya hata mijadala katika ukumbi. Kwa namna hiyo Umoja wa nchi za Ulaya  hutumia kuwasiliana, mazungumzo na maagizo ya programu kwa ajili ya utaratibu wa utendaji wa mwaka unaofuata.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican  

 








All the contents on this site are copyrighted ©.