2017-08-14 09:06:00

Wasiwasi wa Maaskofu nchini Cameroon kutokana na malumbano!


Mazungumzo na madaraka ndivyo viungo vinavyotakiwa kwa pamoja  ambayo Askofu Samuel Kleda, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki wa Cameroon amelekeza,mbele ya hali halisi ya mvutano  ambao  kwa muda mrefu sasa upo katika nchi hiyo baina ya Jumuiya zinazozungumza Kingeraza na zile za Kifaransa.Tangu Novemba 2016 Mikoa ya lugha za kingereza katika nchi Kaskazini Magharibi  na kusini Magharibi ambayo ni takaribani asilimia 20 ya idadi ya watu wamefarakana na kujitenga na Cameroon, hasa ambao wanazungumza kifaransa. Wanao zungumza kingreza wanataka kuunda serikali yao wenyewe , wakiwa na makao makuu ya mji wa Bamenda, ambao zamani ulikuwa ni makao makuu ya wilaya ya Kaskazini Magharibi.

Bila kuunga mkono sehemu yoyote Askofu anasisitiza juu ya mazungumzo kati ya wanao zungumza Kingereza na Kifaransa, hasa haja ya utekelezaji wa sera halisi za kisasa  kwa watawala ili kuweza kuruhusu kila eneo kujiendeleza. Ujumbe kutoka kwa Baraza la Maaskofu hao unaonesha nia ya kutaka kufanya ziara kueleleka Bamenda ili kukutana na wahusika  wanachama wa kingreza. Hata Askofu msaidizi wa Bamenda Michael Ebibi, anarudia kusema kuwa Kanisa ni kinyume na vurugu zozo mahali ambapo zinaweza kujitokeza. Katika msingi wa ombi la kujitenga, kwa kiasi fulani unaweza kuleta aina fulani ya ubaguzi kijamii, kisiasa ingawa  wanachi wa lugha ya kingereza wanadai kuwa na uzoefu wa Cameroon. Katika kusisitiza juu ya uhuru mfano kumeanzishwa kirahisi  ombi la usawa kwa lugha kati ya Kingereza na Kifaransa katika sekta ya Utawala. Kwa njia hiyo Mwezi Januari mwaka huu rais Paul Biya aliamuru kuundwa wa kwa tume ya taifa kwa ajili ya kukuza  lugha mbili na tamaduni nyingi. Lakini pamoja na hayo yote haikutosha kuleta utulivu na mvutano , hadi kufikia baadhi ya wanaotaka kujitenga katika Kamati ya Taifa ya uhuru wa  Kusini  mwa Kamerun (SCNC na  wanachama wanaoongea kifarasa ,walitiwa mbaroni na wengine kurudishwa makwao.

Cameroon ilikuwa koloni la Ujerumani hadi Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Baada ya Ujerumani kushindwa vita, nchi ikagawiwa kati ya Uingereza na Ufaransa chini ya mamlaka ya Shirikisho la Mataifa kama eneo la kudhaminiwa. Mwaka wa 1960, Wafaransa waliacha Kamerun ikawa nchi huru, na kuungana na sehemu ya kusini ya Cameroon ya Kiingereza mwaka 1961 kuunda Shirikisho la Jamhuri ya Kamerun.
Baadaye jina likabadilishwa kuwa Jamhuri ya Muungano ya Kamerun mwaka wa 1972, halafu tena Jamhuri ya Cameroon (kwa Kifaransa République du Cameroun) mwaka wa 1984. Wakazi walikuwa 22,534,532 mwaka 2013, ambao wamegawanyika sawasawa kati ya wanaoishi mijini na wale wa vijijini. Lugha rasmi ni Kifaransa pamoja na Kiingereza. Hata hivyo wakazi wanaongea pia lugha za makabila yao mengi. Upande wa dini, 70% ni Wakristo (40% Wakatoliki na 30% Waprotestanti), 18% ni Waislamu, 3% ni wafuasi wa dini asilia za Kiafrika. 6% hawana dini yoyote.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.