Ijumaa tarehe 8 Septemba 2017 wanawake karibia elfu tano wote wakiwa wanatazamiwa kuvaa nguo za rangi ya machungwa wanatarajia kumpokea Baba Mtakatifu Francisko huko Villavicencio wakati wa Ziara yake ya kitume nchini Colombia, kwa ajili ya kuonesha wazi kampeni ya kupambana na unyanyasaji dhidi ya wanawake. Ni mashirika 30 ya vyama vya wanawake wa nchi walioanzisha mpango huo kama unavyoonesha katika Tovuti ya Kanisa la Colombia kati ya matukio ya Ziara ya Baba Mtakatifu Francisko. Wametengeza tangazo linaoonesha kauli mbiu yao isemayo “sisi wanawake wa Villavicencio,na katika dunia tunapiga hatua mbele kwa ajili ya kutaka uhuru wa maisha dhidi unyanyaswaji”.
Mwakilishi wa chama cha“El Meta na mirada de Mujer”, Nancy Gómez Ramos, amefafanua
lengo la mpango wa kuanzisha suala hilo linalokwenda sambamba na ziara ya Baba Mtakatifu
Francisko ya kwamba ni kutaka kumshirikisha katika mapambano dhidi ya unyanyasaji
wa wanawake ambapo kutoka katika eneo la Villavincencio wanakuza heshima kwa ajili
ya haki ya idadi ya wanawake mahalia na katika dunia kwa ujumla.
Hali kadhalika hata mwakilishi wa Chama kingine cha wanawake kiitwacho Comuna Tres
cha Villavicencio, ameeleza ya kuwa, kwa njia ya vyama hivyo, wanachama wote wanayo
matumaini ya kufungua uwanja mpana ndani ya ziara ya Baba Mtakatifu ili kuweza kuonesha
wazi nafasi na wajibu wa wanawake katika mchakato wa kupunguza vurugu nchini Colombia.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |